English Kiswahili

Ziara ya balozi wa Marekani Nchini Tanzania katika Makumbusho (Iringa Boma)

Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Dk. Donald Wright na familia yake na watumishi wengine wa serikali walitembelea makumbusho ya Mkoa Iringa Boma ilikujifunza historia ya Nchi Tanzania na uhehe tangu kabla na mada ya uhuru.

Mbali na kutembelea Makumbusho ya Mkoa ya mkoa mhe. Balozi alipata kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na mradi wa fahari ytu Tanzania ikiwa ni shemu ya kutangaza utalii wa Tanzania,

Iringa boma imekuwaikipokea wageni mbalimbali wakitaifa na kimataifa wanaokuja kujifunza tamaduni mbalimbali na kupata historia za nchi yetu ilikuendelea kuweka mahusiano mazuri kati ya nchi na nazao.

Karibuni sana makumbusho ya Mkoa Iringa Boma kituo cha Utamaduni.

Uzinduzi wa Mkakati wa Kutngaza Utalii Kusini Mwa Tanzania

Tareherhe 25 hadi 26 mwezi august mwaka 2022 ulifanyika uzinduzi rasmi wa kutangaza utalii kusini mwa Tanzania, uzinduzi huu ulifanyika katika viwanja vya halimashauri ya Mji wa Njombe ambapo Mgeni rasmi wa Uzinduzi huo alikuwa waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania Mhe.Dk. Pindi Chana na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali kama wa Bunge, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.

Mkutano huu ulifanyika sambamba na tamko la Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hasan kutaka kurudishwa kwa maonesho ya karibu kusini na kutangaza vivutio vinavyopatikana kusini mwa Tanzania, aliyesema hayo alopokuwa Iringa Mjini wakati wa Uhamasishaji wa Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka huu.

Mradi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya mkoa Iringa Boma kama wadau wa kubwa wa utalii Tanzania tulifanikiwa kuhudhuria uzinduzi huo na kutoa mchango wetu kama watalaam wa maswala ya Utalii Tanzania.

Ukanda wa kusini mwa Tanzania unajumuisha Mikoa mingi kama vile Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Mtwara na Songwe. Mikoa hii imebarikiwa kuwa na vivutio vya kila aina kama vile Magofu ya kale Mtwara, hifadhi ya Taifa Ruaha na Makumbusho mbalimbali.

 

 

 

 

Mpalano Festival Tukuyu-Mbeya

Mgeni rasmi Chifu Joel Mwakatumbula akitoa pongezi zake za dhati kwa mhifadhi mkuu wa makumbusho ya Mkoa Iringa Boma mara baada ya kutembelea banda letu la maonesho siku ya Mpalano Festival.

Mpalano nineno kutoka kabila la Kinyakiyusa, kabila maarufu Mkoani Mbeya, neno Mpalano tafsiri yake ni tujumuike kwa Pamoja neno hili limetumika katika kuanda maonesho yenye tija kwa nyanda za Juu Kusini na yenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nyanda za Juu kusini.

Mradi wa fahari yetu Tanzania na makumbusho ya Mkoa Iringa Boma kama wadau wakubwa wa utalii Tanzania na nyanda za juu kusini tulipata nafasi ya kushiriki kwenye shughuli hii iliyo fanyika kwa mara ya kwanza Wilaya ya Tukuyu Mkoani Mbeya.

Mradi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya mkoa unatoa shukrani na pongezi dhati kwa wote waliotembelea banda letu la maonesho kwa siku zote tulizo shiriki kwani ni moja kati ya kutngaza utalii wa nyanda za juu kusini.

Utafiti wa Zana za Kale Engaruka ( Arusha-Tanzania)

Watafiti kutoka nchini Ujerumani kwa kushirikiana na mradi wa fahari yetu Tanzania ambao unasimamia makumbusho ya mkoa wa iringa (Iringa Boma ) walitembelea makabila mbalimbali wakati wakifanya utafiti wa zana tofauti zinazotumika katika makabila tofauti nchini Tanzania.

Jamii ya wamaasai katika eneo la Engaruka wilayani Monduli ,jijini Arusha kaskazini magharibi mwa Tanzania ni moja ya kabila ambalo lilifikiwa na watafiti hawa waliohitaji kujua na kujifunza kwa kina juu ya zana mbalimbali ambazo zilitumika kabla na hata baada ya ukoloni..

katika kufanikisha utafiti huo vijana wa jamii ya maasai walikuwa katika mstari wa mbele  kutoa ushirikiano wa karibu katika kufanikisha utafiti huo wenyedhumuni la kujua historia na asili ya zana mbalimbali za makabila tofauti ambazo ziliichukuliwa wakati wa ukoloni wa ujerumani .

Maadhimisho ya Siku ya Chuo Kikuu cha Iringa

 

Chuo kikuu cha Iringa kilifanya maadhimisho yake kwasiku mbili mfululizo tarehe 13.7 Na tarehe 14.7.2022. Maadhimisho hayo yalitanguliwa na maandamano yaliyoanza siku ya kwanza katika viwanja vya Chuo kikuu cha Iringa nakufika katika Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma, ambapo walimu, wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo walipokelewa na Makamu Mkuu wa chuo Prof. Ndelilio Urio katika Makumbusho, kisha kutembezwa  nakupewa masimulizi na wafanya kazi wa makumbusho.

Kilele cha siku ya chuo Kiuu cha Iringa kilitamatishwa siku ya pili katika viwanja vya chuo ambapo Mgeni rasmi wa maadhimisho alikuwa ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Adolf Mkenda pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa sambamba na wageni wengine.

Chuo kikuu cha Iringa ni moja kati ya wadau wakubwa wa makumbusho ya Mkoa Iringa kama ilivyo elezwa kwa undani kupitia tovuti yetu ya fahari yetu Tanzani.

Iringa Boma Easter Market 2023

08. Apr 2023 to 09. Apr 2023

Iringa Boma Easter Market

Iringa Boma Easter Market 2022

16. Apr 2022 to 16. Apr 2022

Easter Market Event

Ufunguzi wa maonesho mapya ya “Mabadiliko ya Binadamu”

05. Dec 2020

Maonesho yaliyosubiriwa kwa hamu pamoja na mambo mengi zaidi...

Jhikoman Reggae Jam Session 2 @Iringa Sunset Hotel

01. Oct 2019

Usikose kumwona tena!

Reggae Live: Jhikoman & Afrikabisa Band

25. Sep 2019

Ni kitu kipya Iringa...

Iringa Boma Siku ya Pasaka 2019

20. Apr 2019

Kwa mara nyingine tena...

Iringa Boma Siku ya Makumbusho Duniani

18. May 2018 to 20. May 2018

maonesho mapya...mitazamo mipya...hadhira mpya...

Iringa Boma Easter Special

29. Mar 2018

Jiandae kwa pasaka!

Iringa Boma Usiku wa Wapendanao

14. Feb 2018

A night to remember!

Ufunguzi Iringa Boma-Makumbusho ya Mkoa & Kituo cha Utamaduni

25. Jun 2016

Ni wakati wa Iringa kung'aa! Kile Kituo cha utamaduni na Makumbusho ya mkoa wa Iringa sasa kitafunguliwa rasmi Juni 25 mwaka huu (2016).

International Summer School: Urithi wa Afrika na nguzo endelevu

25. Jul 2016 to 31. Jul 2016

Kuiweka Iringa kwenye ramani ya masomo ya Urithi wa dunia