conference pic

Kuendeleza na kushirikisha wenyeji katika ulinzi na matumizi ya urithi wa asili na utamaduni ni moja ya kati ya mambo makuu ambayo pia yameibukia katika  masomo ya kimataifa ya masuala ya urithi na usimamizi wake. Lakini hatahivyo, mijadala mbalimbali imeonesha kuwa bado, bara la Afrika halina uzoefu wa kutosha katika mitazamo ya urithi endelevu na maendeleo. Hii ndio sababu chuo kikuu cha Brandenburg Technical University Cottbus-Senftenberg, cha nchini Ujerumani kupitia  kitengo chake cha mafunzo ya uzamili ya masuala ya urithi (The International Graduate School: Heritage Studies) kwa kushirikiana na mradi wa fahari yetu chini ya  chuo kikuu cha  Iringa, Tanzania kutoa nafasi ya kozi hii ya majira ya joto ilikuchangia matamko na mitazamo mbalimbali zaidi ya iliyopo sasa.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mjadala / kozi hii, ingia hapa: http://heritagestudiesafrica.wordpress.com