SiTE ni moja ya tamasha makubwa lilnalofanyika nchini Tanzania kila mwaka kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani na kutafuta wa wekezaji wapya kwenye sekta ya utalii na hata nnje ya utalii, Kwa mara ya sita sasa Tamasha hili limefanyika Nchini tangu kuanzishwa kwake.

Mwaka 2022 Tamasha hili limefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es laam ikiwa ni miaka miwili imepita bila kuwepo kwa Tamasha hili nchini kwa sababu za Uviko-19. Mradi wa fahari yetu Tanzania na Mkaumbusho ya mkoa Iringa tulipata nafasi ya kuhudhuria  kuonesha, kutangaza na kueleza watu malengo ya Mradi.

Mhe.Dk, Philip Mpango Makumu wa rais wa Nchini Tanzania alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Tamasha la  swahili international expo 2022, sambamba na waziri wa Utalii, naibu waziri wa utalii wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa ni miongoni mwa watu walio hudhuria katika maonesho hayo.