Tareherhe 25 hadi 26 mwezi august mwaka 2022 ulifanyika uzinduzi rasmi wa kutangaza utalii kusini mwa Tanzania, uzinduzi huu ulifanyika katika viwanja vya halimashauri ya Mji wa Njombe ambapo Mgeni rasmi wa Uzinduzi huo alikuwa waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania Mhe.Dk. Pindi Chana na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali kama wa Bunge, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.

Mkutano huu ulifanyika sambamba na tamko la Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hasan kutaka kurudishwa kwa maonesho ya karibu kusini na kutangaza vivutio vinavyopatikana kusini mwa Tanzania, aliyesema hayo alopokuwa Iringa Mjini wakati wa Uhamasishaji wa Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwaka huu.

Mradi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya mkoa Iringa Boma kama wadau wa kubwa wa utalii Tanzania tulifanikiwa kuhudhuria uzinduzi huo na kutoa mchango wetu kama watalaam wa maswala ya Utalii Tanzania.

Ukanda wa kusini mwa Tanzania unajumuisha Mikoa mingi kama vile Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Mtwara na Songwe. Mikoa hii imebarikiwa kuwa na vivutio vya kila aina kama vile Magofu ya kale Mtwara, hifadhi ya Taifa Ruaha na Makumbusho mbalimbali.