fahari yetu ni nini?

fahari yetu Tanzania ni mradi ulioanzishwa na ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya. Lengo lake ni kusaidia katika kuondoa umasikini na kuleta maendeleo katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania kupitia kuhifadhi, kuendeleza na kutangaza rasilimali za utamaduni.

Ili kutimiza malengo makuu ya program, fahari yetu umegawanywa katika malengo mkakati matano,  yaliyo katika kamati ya kuendeleza urithi wa dunia ya shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi,  Elimu na Utamaduni (UNESCO) ambayo ni :

  1. Kuaminika kupitia shughuli za utafiti wa kisayansi;
  2. Kuhifadhi, kupitia kuhifadhi nyaraka na maonesho ya wazi;
  3. Kukuza taaluma, kupitia kujenga  uwezo kwa kuendeleza watalaam wa ndani.
  4. Kuwasiliana, kupitia kukuza na kuendeleza biashara;
  5. Kushirikisha jamii, kupitia uhamasishaji na uwezeshaji.

Malengo mkakati matano (The five C’s) ndio yanayounda nembo ya fahari yetu inayorembeshwa na rangi za bendera ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Matokeo tarajiwa ya Mradi

  • Kuziwasilisha, kuzitafsiri, kuchora ramani  na kuziwekea kumbukumbu rasilimali za kitamaduni ili kuhifadhi urithi wa mkoa wa Iringa
  • Kuhakikisha kuwa maeneo na bidhaa za kitamaduni yanaoneshwa na kufikiwa kwa urahisi na umma

  • Kuona urithi wa utamaduni wa ndani, ukitangazwa na kuendelezwa kibiashara
  • Kuona kunakuwa na nguvukazi,  ushindani wa kitaaluma na kijasiriamali  utakaopelekea usimamizi imara wa urithi wa utamaduni na utalii kaika mkoa wa Iringa
  • Kuhakikisha kuwa jamii inafahamu faida za kimazingira, kijamii, na kiuchumi za kutumia na kutunza rasilimali za urithi wa utamaduni