Umepita miaka miwili tangu kuaharishwa kwa tamasha la karibu kusini kutokana na kuwepo kwa janga la Uviko 19 Tanzania na Duniani kwa Ujumla. Mwaka 2022 kumekuwana athari ndogo zinazo sababishwa na Janga la Uviko-19 hivyokupeleka kufanyika kwa Tamasha la Karibu Kusini mkoani Iringa.
Tamasha na maonesho ya karibu kusini yenye lengo la kutangaza utalii uliopo kusini mwa Tanzania limefanyika rasmi kwa siku tano mfululizo Mkoani Iringa katika viwanja wa Kihesa kilolo ambapo maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Mhe.balozi Pindi Chana Waziri wa Maliasili na Utalii Tanzania na kudhuriwa na wa kuu wa mikoa mbalimbali, wakuu wa wilaya, Meya, Viongozi wa kisrikali pamoja na wadau wa Utalii.
Wakati wa uzinduzi rasmi Waziri Pindi Chana amesema kuwa lengo la wiazara ya maliasili na utalii ni kuhakikisha wanapata watalii Milioni Tano na Dollar Millioni mia Tano za Kimarekani kupitia uatalii kusini mwa Tanzania hadi kufikia mwaka 2025.
Madhimisho hayo yalifungwa rasmi siku ya Ijuma na Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibari Mhe Othman Masoud Othman ambeye alikubari kuwa balozi wa Utalii kusini mwa Tanzania kwa hiari na kuahidi kutangaza vivutio vinavyopatikana kusini kupitia lango la utalii lililopo Zanzibari.
Maonesho hayo yaliikutanisha mikoa kumi ianayo patikana kusini mwa Tanzania ikiwemo mkoa wa Mtwara,Njombe,Mbeya,Ruvuma,Iringa,Songwe nk.
Mradi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa – Boma tulipata nafasi ya kuonesha kazi zetu na kutangaza makumbusho ya mkoa kama ilivyo kawaida ya maonesho mengine asanteni sana kwa mliofika kutebelea banda letu na kufika katika Makumbusho yetu.