Kama ilivyo kawaida ya makumbushoya mkoa Iringa-Boma kila baada ya miezi mitatu hufanya tukio Fulani lenye kuelimisha au kuenzi utamaduni mwaka 2022 kulifanyika maonesho ya vyakula asili katika makumbusho ya mkoa Iringa Boma ikiwa ni kwa mara ya kwnza tangu kuanzishwa makumbusho hii.

Lengo kubwa la kufanya maonesho ya vyakula asili ilikuwa ni kuenzi, kukumbusha na kuelimisha watu kuhusu vyakula vyetu vya asili, kwani katika maonesho hayo watu walipata kujifunza namna kuandaa vyakula hivyo kuanzia hatua ya awali hadi ya mwisho lakini pia watu wote walipata nafasi ya kuonja vyakula na vinywaji hivyo vya asili.

Viazi vitamu , Ugali, Mkande, ni baadhi ya vyakula ambavyo vilikuwepo Ulanzi Msabe na matunda mbalimbali ya Asili yanayopatikana nyanda za juu kusini.

Makumbusho ya Mkoa na Mradi wa fahari yetu Tanzania tunatoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote waliofanikiwa kufakia na kufanikisha tukio hili tunawakaribisha tena katika matukio mengine yanayo fuata.