Maonesho haya hueleza asili na mabadiliko ya mwanadamu na tamaduni zake, hasa mkoa wa Iringa. Yanawakilisha utajiri wa urithi wa historia ya kale na ugunduzi huu huchochea mijadala katika elimu ya mabadiliko ya binadamu ulimwenguni na umuhimu wa vituo hivyo kama vivutio vya utalii. Pia, utengengenezaji wake umewajengea uwezo wafanyakazi wa Iringa Boma pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu tofauti nchini Tanzania. Ufunguzi unaambatana na ngoma za asili, bendi ya mziki wa kisasa, fashion show, na vyakula na vinywaji hadi usiku.

Maonesho na tamasha la kitamaduni yamedhaminiwa na Gerda Henkel Stiftung na Stiftung Nord-Süd-Brücken nchini Ujerumani.

Matukio ya Kitamaduni

Maonesho ya Utamaduni & Historia