1. Ni wakati wa Iringa sasa kungaa!

Kituo cha Urithi wa Utamaduni na Makumbusho ya mkoa yatafunguliwa rasmi  Juni 25, 2016.
Kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayoambatana na ufunguzi ikiwemo maonesho ya kitamaduni na sherehe rasmi za ufunguzi. Tunawakaribisha wakazi na watanzania wote kuja kusheherekea utamaduni na historia ya nyanda za juu kusini.

Pamoja na maonesho mbalimbali ya kuvutia ikiwemo Historia ya Iringa, Uganga na tiba asili, Hazina na asili ya Utamaduni wa Mkoa wa Iringa, pia kuna jambo la ziada la kujifunza kwa kila mtu.

Tafadhali jiunge nasi na kuona matokeo ya miaka kadhaa ya kazi ya kujitolea ya kulifufua Boma la iringa na kulifanya kuwa alama ya kipekee  kusini mwa Tanzania.
Karibu Sana

20160226-144837