Maandalizi ya Makala ya kumbukizi ya Ukoloni, Tanzania

Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma imepata nafasi ya kushiriki kwenye uandaaji wa Makala ya redio ya Shirika la Utangazaji la Ujerumani kuhusu kumbukumbu ya Historia ya kikoloni nchini Tanzania kwa kuangazia namna gani wananchi wanaikumbuka na jitihada za taasisi hususan Makumbusho wanavyoitunza Historia hiyo.

Kulia ni Bwana, Jochen Rack kutoka Shirika la Utangazaji Ujerumani (Bavaria Broadcast Corporation)

Tanzia Mhe. Balozi Dkt. Augustine P. Mahiga

Dkt. Augustine Philip Mahiga, Balozi na Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefariki dunia leo alfajiri 01 Mei, 2020 Jijini Dodoma.

Daima tutakumbuka na tutamenzi Dkt. Mahiga kama Balozi wa fahari yetu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kama Balozi wa Mkoa wa Iringa na watu wake kwa dunia nzima. Tangu alipofungua rasmi Makumbusho ya Mkoa wa Iringa Boma mwaka 2016, alitushauri na kutuongoza ktk kuendeleza kazi yetu na kuitangaza kitaifa na kimataifa. Tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi. Tunapenda kutoa salamu za rambirambi za dhati kwa familia na ndugu yake pamoja na watu wote walio karibu naye.