Utafiti Mkoa wa Tabora

Mradi wa fahari yetu Tanzania kwa kushirikiana na makumbusho ya Ujerumani wame anza utafiti wake wa kihistoria na mambo kale kwa baadhi ya mikoa hapa Nchini.

Mradi ume anza utafiti rasmi katika mkoa wa Tabora ambapo wametembelea majengo ya kihistoria kama Boma ya Mjerumani, Makumbusho ya Dr.Living Stone na baadhi ya machifu mkoani hapo kama Chifu Isike Mwanakiyungi, Mtemi Mirambo na Chifu Lugusha.

Lengo kuu ni kupata historia na kuangalia zana mbalimbali za kale zilizopo kwa kulinganisha na zile zilizopo Makumbusho ya Ujerumani ili kujifunza zana hizo zilichukuliwa wapi na zilikuwa na matumizi gani.

Uzinduzi wa Maonesho Mapya ya Masimulizi ya Kiasili ya Kusisimua.

Makumbusho ya mkoa – Iringa Boma imezindua maonesho mapya ya Masimulizi ya kiasili ya kusisimua yenye lengo la kuhifadhi na kurithisha masimulizi na hadithi zilizopo kwenye hatari ya kupotea kwenye jamii ya sasa.

Maonesho hayo yalizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa Iringa Mh. Queen Cuthbert Sendiga pamoja na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya, Manispaa, Wazee wa kimila na wageni wengine.

 

 

 

Maonesho ya vyuo vikuu Tanzania Mnazi Mmoja

Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma na Mradi wa fahari yetu Tanzania kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Iringa tumepata nafasi ya kushiriki maonesho ya vyuo vikuu Tanzania yanayo fanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es salaam. Tupo kwenye banda la Chuo Kikuu Iringa karibu upate kuifahamu historia ya Mkoa wa Iringa kwa ufupi.