Ni takribani miaka mi tatu ilipita bila kufanikisha tukio la Easter market katika viwanja vya makumbusho, sababu kubwa ilikuwa Ni ugonjwa wa Uviko 19 uliopelekea kupigwamarufuku kwa mikusanjiko ya watu, mikutano na shughuli mbalimbali zenyeuhitaji wa watu wengi.

Mwaka 2022 umekuwa mwaka wenye bahati kwakufanikiwa kufanya Event hii iliombatana na uzinduzi wa mgahawa wetu Aroma Coffee House @boma, licha ya tukio kupita lakini Mgahawa umeanza kufanya kazi rasmi.

Uongozi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma unatoa shukrani zake za dhati kwa wote walio fanikisha kufanyika kwa tukio hili na wale walio hudhulia siku ya tukio. Uongozi wa mradi unawakaribisha tena kwenye matukio mengine yatakayokuwa yanaendelea, kwani mwisho wa tukio moja ndio mwanzo wa matukio mengine.

Hapo zamani mfumo wa utawala wa kikoloni uliigawa Tanganyika (Tanzania) kwenye majimbo makubwa nane (8), Jimbo la Kusini ambalo lilijumuisha Mikoa ya Ruvuma,Lindi, na Mtwara amabapo makao makuu yalikuwa lindi.

Mwaka 1971 ndipo ulipo anzishwa Mkoa wa Mtwara, kuanzishwa kwa  Mkoa huu kulitokakana na mpango wa Madaraka Mikoani ulio simamiwa na Rais wakwanza wa Tanzania Mwl.Julius.K. Nyerere uliokuwa na lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.Tafsiri ya neno “NTWARA” ambalo kwasasa ni Mtwara linatokana na neno la kimakonde “kutwara” lenye maana ya ku-twaaliwa (kuvamiwa na kuchukuliwa mateka).

Asilimia 75 ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara ni Wamakonde.  Wayao na Wamakua miongoni mwa makabila yanayo patikana katika mkoa huu. Mradi fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma tulifanikiwa kufika Mtwara kwa lengo la utafiti, Mikindani,Mtwara mjini, Tandahimba na Newala ni baadhi ya maeneo tuliofanikiwa kufika wakati wautafiti.

Lindi Ni miongoni mwa mikoa inayopatikana Tanzania ni moja kati ya Mikoa mikongwe ilioanza kati ya karne ya 11 kwenye historia ya Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Historia ya Mkoa wa Lindi inapambwa na badhii ya maeneo yaliopo kwenye wilaya za Mkoa huo. Jina la Lindi maana yake ni SHIMO REFU, Bandari ya Lindi ilitumika katika kusafirishia watumwa kutoka Ziwa Nyasa. Waarabu waliofika karne ya 18, wahindi,wajerumani na waingereza ni miongoni mwa mataifa yaliyofanikiwa kuishi katika mkoa huu.

Mradii wa fahari yetu Tanzania na makumbusho ya Mkoa Iringa Boma tulifanikiwa kufika katika mkoa wa Lindi kwa ajili ya utafititi wa mambo kale na zana za asili zilizo tumika na wazawa tangu miaka 100 iliyopita. Lindi mjini, Kilwa Kipatimu (Nandete), Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani Songo Mnara (Mji wa kale wa kiaarabu), Kilwa Masoko na Nchinga ni baadhi ya maeneo tuliyofanikiwa kuetembelea na kufanya utafiti katika mkoa wa Lindi.

 

Mradi wa fahari yetu Tanzania umesaidia na kuchangia matembezi ya kitaaluma ya siku nne ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wanaosoma Shahada ya kwanza ya Utamaduni Antropolojia na Utalii kozi ya uhusiano wakimataifa, walioenda kutembelea baadhi ya balozi za mataifa mbalimbali nchini Tanzania na baadhi ya ofisi  zilizopo Dar es laam, kwalengo lakujifunza kwavitendo.

Baadhi ya balozi hizo ni kama Ubalozi wa Ujerumani, Ubalozi wa Ungereza,ubalozi wa Ufaransa, Ubalozi wa Uturuki, ofisi za Umoja wa Ulaya (EU), ofisi za IMF, Pamoja na kutembelea uwanja ndege wakimataifa wa mwalimu Julius Nyerere.

.

Mradi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma tulitembelewa na mgeni kutoka ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania. Tumefurahia ujio wako kwenye makumbusho ya Mkoa Iringa Boma tunaamini ni mengi umejifunza siku ya leo kupitia makumbusho hii.