Makumbusho ya Mkoa wa Iringa na Kituo cha Utamaduni yamefanya utafiti maalum unaolenga kukusanya na kuhifadhi maarifa ya jamii kuhusu wanyama na uwindaji sehemu muhimu ya urithi wa kitamaduni wa eneo hili. Utafiti huu unachunguza namna jamii zilivyofaidika na wanyama, hadhi ya wawindaji hodari, pamoja na maana za kitamaduni zinazohusishwa na wanyama, huku pia ukiangazia athari za ukoloni katika mifumo hiyo.

Utafiti ulifanyika katika maeneo ya Tarafa ya Pawaga (kijiji cha Mbugani), Itunduma katika Wilaya ya Kilolo, na kijiji cha Pomerini. Kwa kutumia mbinu ya historia simulizi, watafiti walishirikiana na wazee wenye heshima kama Lukinga, Yassin Stambuli Mwilinge, Hasheem Nguki, Shaban Omari Swila Ndele, Msungu, Menda, Merckzedeck Ngakonda, na Mzee Luoga. Ushuhuda wao ulitoa mwanga muhimu kuhusu mifumo ya jadi ya uwindaji na mabadiliko yake kwa nyakati tofauti.

Matokeo yanaonesha kuwa uwindaji haukuwa kwa ajili ya chakula pekee, bali pia ulikuwa ishara ya ujasiri, ustadi, na uongozi. Bidhaa za wanyama kama ngozi na mafuvu zilikuwa na umuhimu mkubwa wa kitamaduni, zikiwakilisha heshima na hadhi ya kijamii. Hata hivyo, ukoloni uliathiri mila hizi kwa kuweka vikwazo vya uwindaji na kuchukua mabaki ya wanyama kama nyara.

Aidha, utafiti ulihusisha utambuzi wa baadhi ya mabaki ya wanyama yaliyochukuliwa wakati wa ukoloni, na kuyarejesha katika muktadha wake wa asili ya kitamaduni. Hii ni hatua muhimu katika kuhifadhi kumbukumbu, kuimarisha utambulisho wa jamii, na kuendeleza mjadala kuhusu urejeshaji wa urithi.

Kupitia kazi hii, makumbusho yanaendelea kutoa jukwaa kwa sauti za jamii na kuhakikisha simulizi hizi muhimu zinaendelea kuwa sehemu ya historia hai ya Iringa.

Kwa mara ya tatu mfululizo, Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma na Kituo cha Utamaduni yamepokea kwa furaha wanafunzi wapatao mia tatu wa kozi ya Utalii kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma. Ziara hii ni sehemu muhimu ya kujifunza kwa vitendo, ambapo wanafunzi wanapata fursa ya kuongeza ujuzi na maarifa yao ya kitaaluma. Hii ni hatua muhimu katika kuwaandaa kwa mafanikio wanapomaliza masomo yao ya chuo.

Mbali na kukuza taaluma za wanafunzi, ziara hizi pia zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kuhamasisha utalii wa kiutamaduni na utalii wa ndani. Kupitia ziara hizi, tunazidi kuthibitisha kwamba utamaduni wetu ni hazina inayoweza kuwavutia watu wa rika na taaluma mbalimbali, na hivyo kuimarisha ushirikiano baina ya sekta ya elimu na utalii.

Tunatoa shukrani za dhati kwa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuendelea kutuchagua kama sehemu ya mafunzo yao ya vitendo. Makumbusho ya Mkoa Iringa ni kielelezo cha urithi wa kihistoria na kiutamaduni uliopo katika Manispaa ya Iringa. Ushirikiano huu ni wa manufaa makubwa, siyo tu kwa wanafunzi, bali pia kwa jamii yetu kwa ujumla.

Kwa moyo mkunjufu, tunawakaribisha tena kuungana nasi wakati mwingine. Tutaendelea kushirikiana kwa karibu katika kutoa elimu na kukuza uelewa kuhusu utamaduni wetu kupitia utalii wa kiutamaduni. Karibuni tena Iringa, mahali ambapo historia na utamaduni vinaishi milele.

Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Iringa Profesa Edward Hosea, alifanya ziara ya kutembelea Makumbusho ya Mkoa wa Iringa Boma, ambayo ni sehemu muhimu ya mradi wa “fahari yetu Tanzania.” Ambao ni mradi uliopo chini ya Chuo Kkuu cha Iringa Katika ziara hiyo, Profesa Hosea alionyesha kujivunia juhudi zinazofanywa na mradi huu katika kukuza vijana katika Nyanja mbalimbali, kuhifadhi utamaduni na kutangaza utalii wa Utamaduni.

Akizungumza katika makumbusho, Profesa Hosea alisema, “Mimi ni mdau mkubwa wa masuala ya utalii. Hongereni kwa kazi yenu ya ukarabati wa jengo hili la kale na uhifadhi uliofanyika mmeweza kurejesha thamani yake, ni wazi kuwa juhudi hizi zina manufaa makubwa kwa jamii na historia ya Tanzania.”

Hata hivyo ameahidi kuunga mkono juhudi zinazofanywa mradi wa “fahari yetu Tanzania” na Makumbusho ya Mkoa wa Iringa Boma, akisisitiza kwamba Chuo Kikuu cha Iringa kitatoa ushirikiano mkubwa ili kuimarisha juhudi za kuhifadhi urithi wa utamaduni.

Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania ili andaa maonesho na kutoa mialiko kwa wadau mbalimbali wa utalii, ikiwemo Mradi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma, maonyesho haya yenye lengo la kuwajengea waheshimiwa wabunge uelewa na kuwapatia elimu kuhusu uhifadhi wa wanyamapori, malikale, na uendelezaji wa utalii nchini maonesho yalifanyika katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma kuanzaia tarehe 30 Mei hadi 3 Juni 2024.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angela Kairuki, alipotembelea banda la Makumbusho ya Mkoa wa Iringa Boma, alitoa pongezi za dhati kwa mradi wa fahari yetu Tanzania kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika kutangaza na kuendeleza utalii wa kiutamaduni. Waziri Kairuki alisisitiza umuhimu wa mradi huu katika kuanzisha na kusimamia makumbusho ya Mkoa wa Iringa, jambo ambalo lina mchango mkubwa katika kuhifadhi na kuendeleza utamaduni wa taifa letu.

“Nimefurahishwa sana na kazi kubwa mnayofanya katika kutangaza utalii wa kiutamaduni,” alisema Waziri Kairuki. “Nimekuwa nikifuatilia taarifa zenu kupitia mitandao ya kijamii kama Instagram, na ni dhahiri kuwa mnachangia kwa kiasi kikubwa katika kuonyesha uzuri na utajiri wa utamaduni wetu kwa dunia nzima.”

Dkt. Jan Kuver, Mkurugenzi wa Mradi wa Fahari Yetu na makumbusho ya Iringa Boma, anaeleza kuwa, Maonyesho haya yaliyofanyika Dodoma ni jukwaa muhimu la kutangaza utalii wa ndani na nje kwa wabunge na wadau wengine wa utalii. Maonyesho haya yanaweza kuongeza chachu ya kutangaza utalii kwa kuwawezesha wabunge na viongozi wengine kuona na kushiriki moja kwa moja katika shughuli za utalii, na hivyo kuboresha uelewa na ushirikiano wao katika kuendeleza sekta hii muhimu. Ushirikiano baina ya Wizara ya Utalii na wadau wengine katika maonyesho haya ni wa manufaa makubwa, kwani unawawezesha kubadilishana mawazo na mbinu bora za kutangaza utalii, na hivyo kuleta ubunifu na ufanisi katika sekta hii.

“Kupitia maonyesho haya, sisi kama fahari fetu Tanzania tumejifunza vingi na kupata fursa ya kukutana na wadau wengi ambao tunaweza kushirikiana nao katika kufanya shughuli za utalii”.

Makumbusho ya mradi wa fahari yetu Tanzania unatoa  shukrani kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaliko huu muhimu.Kwani umetuwezesha kuelezea shughuli zinazofanywa na makumbusho na kutoa fursa ya kutangaza utalii kwa waheshimiwa wabunge. Tunatumaini kuwa wabunge hawa watakuwa mabalozi wa kutangaza utalii unaopatikana Iringa katika majimbo wanayowakilisha.

Maonesho ya pamoja ya Mradi wafahari yetu Tanzania na Kibubu Ufinyanzi yamefanyika kwa mafanikio makubwa katika viwanja vya Nafasi Art Space Mikocheni B jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Januari 2024. Mradi wa wafahari yetu Tanzania uliwasilisha maonesho ya “Endangered Story of Enchanted Place Phase II, huku Kibubu Ufinyanzi wakionyesha ubunifu wao katika kufinyanga vitu vyenye naumbo mbalimbali kwamatumizi ya  kuhifadhi fedha..

Maonesho haya yalikuwa ni matokeo ya ufadhili ambao waliipokea kutoka Nafasi Art Space mwaka mmoja uliopita. Dkt. Noel Lwoga, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maonesho haya, alitoa maoni yake akisema, “Ni vyema kutangaza utalii kwa njia tofauti”. Tumeona mradi wa wafahari Yetu Tanzania wameamua kuleta simulizi zilizomo katika jamii zetu. Simulizi hizi zenye kuibua hisia kwa watu, ingawa zinaweza kuonekana kama za kufikirika lakini nisimulizi zakweli na zenye kusisimua.

Mkurugenzi wa Nafasi Art Space aliongezea kwa kusema kuwa wamefurahi kuona mafanikio ya ufadhili waliotoa na kuwakaribisha wanasanaa wengine kuomba ufadhili. Hama hivyo. Dkt. Jan Kuver, Meneja wa mradi wa fahari yetu Tanzania, alielezea kuwa maonesho haya yalikuwa ya pili, baada ya yale yaawali kufanyika Iringa na sasa yamehamishiwa Dar es Salaam. Pia, wanaendelea kuandaa vitabu vyenye picha za kuchora kwa ajili ya kusambaza mashuleni ili kuendelea kuhifazi msimulizi haya kupitia kwa watoto.

Maonesho haya yamekuwa ni fursa nzuri ya kukuza utamaduni, ubunifu, na kuelimisha jamii kuhusu mambo mbalimbali yanayowahusu. Tunatarajia kuona juhudi kama hizi zikiendelea na kuchochea maendeleo katika sekta za utalii na sanaa nchini Tanzania.