Utafiti Jiji la Mwanza

Hatimaye tumefanikiwa kumaliza utafiti wetu katika Jiji la Mwanza. Hapa Mwanza tumefanikiwa kutembelea Makumbusho ya Bujora (Sukuma Musem), kituo cha gari moshi Mwanza chenye miaka zaidi ya mia na kenda,jengo la Mjerumani pamoja na wazee wa Mwanza walitupa masimulizi zaidi huku tukijionea kazi za mikono zilizokuwa zikifanywa hapo zamani kama ufinyanzi.

Ni mengi tume jifunza na tumefanikisha utafiti wetu kwa kiasi. Shukrani kwa wote walio tusaidia kwenye utafiti wetu.

Utafiti Mkoa wa Kagera

Kuna mengi tuli jifunza hapa Kagera ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa utamaduni wao hasa wa matumizi ya lugha ya asili, Pia tulipata fursa ya kufanya utafiti wetu kwa siku kadhaa kwenye falme za Buhaya chini ya watemi kama Mkama Kahigi,Mtemi Lukamba na Mtemi wa Karagwe.

Hata hivyo tulitembelea Makumbusho ya Kagera kujifunza na kujionea uhifadhi wa zana za kale zilizo hifadhiwa hadi leo.

Utafiti Mkoa wa Tabora

Mradi wa fahari yetu Tanzania kwa kushirikiana na makumbusho ya Ujerumani wame anza utafiti wake wa kihistoria na mambo kale kwa baadhi ya mikoa hapa Nchini.

Mradi ume anza utafiti rasmi katika mkoa wa Tabora ambapo wametembelea majengo ya kihistoria kama Boma ya Mjerumani, Makumbusho ya Dr.Living Stone na baadhi ya machifu mkoani hapo kama Chifu Isike Mwanakiyungi, Mtemi Mirambo na Chifu Lugusha.

Lengo kuu ni kupata historia na kuangalia zana mbalimbali za kale zilizopo kwa kulinganisha na zile zilizopo Makumbusho ya Ujerumani ili kujifunza zana hizo zilichukuliwa wapi na zilikuwa na matumizi gani.

Uzinduzi wa Maonesho Mapya ya Masimulizi ya Kiasili ya Kusisimua.

Makumbusho ya mkoa – Iringa Boma imezindua maonesho mapya ya Masimulizi ya kiasili ya kusisimua yenye lengo la kuhifadhi na kurithisha masimulizi na hadithi zilizopo kwenye hatari ya kupotea kwenye jamii ya sasa.

Maonesho hayo yalizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa Iringa Mh. Queen Cuthbert Sendiga pamoja na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya, Manispaa, Wazee wa kimila na wageni wengine.