Mradi wa fahari yetu Tanzania kwa kushirikiana na makumbusho ya Ujerumani wame anza utafiti wake wa kihistoria na mambo kale kwa baadhi ya mikoa hapa Nchini.

Mradi ume anza utafiti rasmi katika mkoa wa Tabora ambapo wametembelea majengo ya kihistoria kama Boma ya Mjerumani, Makumbusho ya Dr.Living Stone na baadhi ya machifu mkoani hapo kama Chifu Isike Mwanakiyungi, Mtemi Mirambo na Chifu Lugusha.

Lengo kuu ni kupata historia na kuangalia zana mbalimbali za kale zilizopo kwa kulinganisha na zile zilizopo Makumbusho ya Ujerumani ili kujifunza zana hizo zilichukuliwa wapi na zilikuwa na matumizi gani.