Chuo Kikuu cha Iringa

Ni chuo kikuu binafsi kilichopo chini ya kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania. Chuo kina wanafunzi takriban 4000 ambao wamesajiliwa katika vitivo vya Sanaa na Sayansi ya jamii, Biashara na Uchumi, Ushauri nasaha na Saikolojia. Vitivo vingine ni Sheria Sayansi na Elimu na Theolojia. Mradi wa Fahari yetu unaendeshwa na Idara ya Utamaduni na Utalii iliyo ndani ya kitivo cha Sanaa na Sayansi ya jamii.

Kutokana na taaluma kubwa iliyonayo katika utafiti, urithi wa utamaduni na utalii, timu ya chuo kikuu cha Iringa inaratibu na kusimamia mradi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuwajibika kwa mfadhili

Chuo Kikuu cha Göttingen, Ujerumani

www.uni-goettingen.de/en

Fahari yetu inashirikiana na Taasisi ya Ethnolojia pamoja na kituo cha utafiti  wa masuala ya jamii kilicho ndani ya chuo hiki cha serikali cha ujerumani. Ushirikiano kati ya fahari yetu na Chuo Kikuu cha Göttingen unasaidia katika kukuza taaluma katika masuala ya urithi wa utamaduni na vilevile kujiongezea uwezo na sifa kupitia semina za kimataifa, kubadilishana walimu, na kwa pamoja kufanya tafiti na maonesho mbalimbali.

Chuo Kikuu cha Lund, Sweden

www.lunduniversity.lu.se

Tangu mwaka 2018, mradi wa fahari yetu na Chuo Kikuu cha Lund cha huko Sweden wamekuwa wakibadilishana wafanya kazi wakitaaluma na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Lund huko Sweden. Mbadilishano huu umeundwa kwalengo la kukuza uwezo wa kitaalama wa wafanyakazi wa makumbusho ya Mkoa Iringa Boma,Katika muundo wa maonyesho na usimamizi wa makumbusho.

 Mkoa wa Iringa

www.iringa.go.tz  / www.pmoralg.go.tz

Mkoa, kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inatoa msaada wa kiutawala, na pia ni kiungo kati ya serikali kuu na serikali za mitaa. Chombo hiki pia kinachukua jukumu  katika kufanikisha ushirikiano kati ya mradi na umma na kutoa misaada ya kiutawala kama vile kuwezesha kufikika kwa maeneo yaliyo katika mradi,kutoa vibali na maeneo kwa ajili ya mradi, kusaidia mradi na vizuizi vya kisiasa, kuandaa matamasha na matukio mengine ya utamaduni

Halmashauri ya Wilaya ya Iringa

www.iringadc.go.tz

Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inausaidia mradi katika kuendeleza utekelezaji wa uhamasishaji jamii,  kuanzisha na kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali  vijijini katika Mkoa wa Iringa .

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa

www.iringamunicipalcouncil.go.tz

Ikiwa ni mwenyeji wa mradi,  ofisi ya Halmashauri ina nafasi na wajibu mkubwa katika kuhamasisha jamii iliyopo katika Manispaa kuthamini, kutunza, kuendeleza, na kuendelea kutangaza kwa watalii maeneo lengwa ya kiutamaduni.

Makumbusho ya Taifa / Nyumba ya Utamaduni

www.houseofculture.or.tz

Makumbusho ya Taifa ni mdau wa makumbusho mbalimbali za Tanzania yenye lengo la kuhifadhi na kuonesha historia na mazingira asilia ya Tanzania. Makumbusho ya Taifa yanausaidia mradi kwa kutoa utaalam na uzoefu wake katika kurejesha upya maeneo ya kitamaduni na maonesho.

Washirika

 Umoja wa Ulaya

eeas.europa.eu/delegations/tanzania_en

Fedha za awali za kuanzisha Mradi wa fahari yetu – Tanzania Heritage & Culture Solutions zilitolewa kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya kupitia Ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania. Ufadhili huo wa mwaka 2013-2016 ulihusisha marejesho na samani za Makumbusho na Kituo cha Utamaduni cha Iringa Boma, miradi ya utafiti na tafsiri ya urithi wa Iringa, shughuli za uhamasishaji na uwezeshaji jamii, maendeleo ya bidhaa za urithi na jitihada za masoko, na hatua za kujenga uwezo katika malikale na utalii. usimamizi.

Ofisi ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani

www.auswaertiges-amt.de/en

Tangu 2015-2016, Ofisi ya Mambo ya Nje ya Shirikisho ilifadhili ukarabati wa jengo la Iringa-Boma  pamoja na uwekaji wa maonyesho ya utamaduni na historia ya kikanda kupitia programu yake ya kuhifadhi utamaduni, inatarajiwa kusaidia shughuli za fahari yetu na Iringa Boma katika awamu nyingine ya ufadhili kuanzia 2020-2021.Ushirikiano huo unaratibiwa kwa karibu na Ubalozi wa Ujerumani Dar es Salaam.

Ubalozi wa Marekani Tanzania

https://tz.usembassy.gov/

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulisaidia Mradi wa  Fahari yetu katika kufanikisha tamasha la Mashindano ya Utamaduni kwa Mkoa wa Iringa, pamoja na ufunguzi rasmi wa Makumbusho ya Mkoa na Kituo cha Utamaduni (Iringa Boma) mwaka 2016.

Wizara ya Maliasili na Utalii

www.mnrt.go.tz

Idara ya Utalii na Idara ya Mambo Kale: Vyombo hivi vya serikali vinauongezea nguvu mradi kwa kusaidia utaalam wa uhifadhi na urejeshaji wa maeneo ya kihistoria (Idara ya Mambo Kale), na kutengeneza, kusimamia na kutekeleza sera ya  utalii na urithi wa utamaduni (Idara ya Utalii).

Hifadhi ya Taifa Tanzania

www.tanzaniaparks.com

Chombo hiki kinauchangia  mradi utaalam wake  katika kukuza utamaduni na masoko ya utalii.

Bodi ya Utalii Tanzania

www.tanzaniatouristboard.com

Chombo hiki pia kinachangia utaalam katika kukuza utamaduni na masoko ya utalii kwa mradi.