Mpalano Festival Tukuyu-Mbeya

Mgeni rasmi Chifu Joel Mwakatumbula akitoa pongezi zake za dhati kwa mhifadhi mkuu wa makumbusho ya Mkoa Iringa Boma mara baada ya kutembelea banda letu la maonesho siku ya Mpalano Festival.

Mpalano nineno kutoka kabila la Kinyakiyusa, kabila maarufu Mkoani Mbeya, neno Mpalano tafsiri yake ni tujumuike kwa Pamoja neno hili limetumika katika kuanda maonesho yenye tija kwa nyanda za Juu Kusini na yenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nyanda za Juu kusini.

Mradi wa fahari yetu Tanzania na makumbusho ya Mkoa Iringa Boma kama wadau wakubwa wa utalii Tanzania na nyanda za juu kusini tulipata nafasi ya kushiriki kwenye shughuli hii iliyo fanyika kwa mara ya kwanza Wilaya ya Tukuyu Mkoani Mbeya.

Mradi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya mkoa unatoa shukrani na pongezi dhati kwa wote waliotembelea banda letu la maonesho kwa siku zote tulizo shiriki kwani ni moja kati ya kutngaza utalii wa nyanda za juu kusini.

Utafiti wa Zana za Kale Engaruka ( Arusha-Tanzania)

Watafiti kutoka nchini Ujerumani kwa kushirikiana na mradi wa fahari yetu Tanzania ambao unasimamia makumbusho ya mkoa wa iringa (Iringa Boma ) walitembelea makabila mbalimbali wakati wakifanya utafiti wa zana tofauti zinazotumika katika makabila tofauti nchini Tanzania.

Jamii ya wamaasai katika eneo la Engaruka wilayani Monduli ,jijini Arusha kaskazini magharibi mwa Tanzania ni moja ya kabila ambalo lilifikiwa na watafiti hawa waliohitaji kujua na kujifunza kwa kina juu ya zana mbalimbali ambazo zilitumika kabla na hata baada ya ukoloni..

katika kufanikisha utafiti huo vijana wa jamii ya maasai walikuwa katika mstari wa mbele  kutoa ushirikiano wa karibu katika kufanikisha utafiti huo wenyedhumuni la kujua historia na asili ya zana mbalimbali za makabila tofauti ambazo ziliichukuliwa wakati wa ukoloni wa ujerumani .

Maadhimisho ya Siku ya Chuo Kikuu cha Iringa

 

Chuo kikuu cha Iringa kilifanya maadhimisho yake kwasiku mbili mfululizo tarehe 13.7 Na tarehe 14.7.2022. Maadhimisho hayo yalitanguliwa na maandamano yaliyoanza siku ya kwanza katika viwanja vya Chuo kikuu cha Iringa nakufika katika Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma, ambapo walimu, wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo walipokelewa na Makamu Mkuu wa chuo Prof. Ndelilio Urio katika Makumbusho, kisha kutembezwa  nakupewa masimulizi na wafanya kazi wa makumbusho.

Kilele cha siku ya chuo Kiuu cha Iringa kilitamatishwa siku ya pili katika viwanja vya chuo ambapo Mgeni rasmi wa maadhimisho alikuwa ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Adolf Mkenda pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa sambamba na wageni wengine.

Chuo kikuu cha Iringa ni moja kati ya wadau wakubwa wa makumbusho ya Mkoa Iringa kama ilivyo elezwa kwa undani kupitia tovuti yetu ya fahari yetu Tanzani.

Maonesho ya siku ya Sabasaba (77) Mkwawa

 

Makumbusho ya mkoa Iringa Boma na Mradi wa fahari yetu Tanzania tulipata nafasi ya kushiriki katika maonesho ya sababa yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo kikuu kishiriki cha Dar es laam Mkwawa, Maonesho hayo yalifunguliwa na Mgeni rasmi Mh.Saad Mtambule Mkuu wa wilaya ya Mufindi Iringa.

Banda la makumbusho ya mkoa Iringa Boma tulipata nafasi ya kutembelewa na Mgeni rasmi wa maonesho haya yaliyofanyika siku ya sabasaba kamailivyo fanyika kwa mabanda mengine, Kutangaza vivutio vya ndani na historia yetu kama watanzania ni moja kati ya vitu alivyo sisitiza mgeni rasmi katika maonesho haya pindi alipo tembelea banda letu.

“Watu wengi wanajua kuwa utalii ni kwenda Mbugani au kupanda mlima Kilimanjaro na kufika katika maeneo ya fukwe, hapana utalii ni Zaidi ya hivi Iringa boma nimependa juhudi zenu katika kutanga utalii wa malekale na historia  lakini tusiishie hap ana tuongeze kasi katika kutangaza utalii huu duniani kote”.

Sikukuu ya sababa illianza rasmi mwaka 1954 tarehe 7 ya mwezi wa 7 baada ya chama cha   TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION (TAA) na AFRICAN ASSOCIATION (AA) kuungana na kupatikana chama cha TANGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION  (TANU), chama ambacho kili saidia katika kudai uhuru wa Nchi yaTanganyika (1960) chini ya mwalimu Nyerere rais wa kwanza wa Tanganyika.

Kwa kuwa sera ya chama hiki ilikuwa ni Kilimo “Kilimo nii utii wa Mgongo” basi watu wengi waliamua kujihusisha na shughuli za kilimo na walipeleka mazao yao kila siku katika maonesho  yakikuwa yakifanyika siku ya tarehe 7 Mwezi wa 7 ilikuenzi muungano huo, kwa hivi sasa sikuku hii ya wakulima imegeuka na kuwa kama siku ya wafanyabiashara.

Ukumbi wa Siasa ni Kilimo ulipo Iringa mjini ni moja kati ya mazao ya sera ya kilimo iliyoanzishwa miaka ya 1954 baada ya kuzaliwa kwa chama cha TANU.

 

 

 

 

Matembezi ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa

Wakati kaitka picha ni Mkurugenzi wa makumbusho ya Taifa Dr. Noel Lwoga alipata nafasi ya kutembelea Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma wakatiakipita Iringa kuelekea Dodoma. Uhifadhi wa malikale kama sehemu ya makumbusho na kituo cha utamaduni na  Masimulizi / historia za wenyeji na Machifu kwa wageni hata wazawa wa Mkoa wa Iringa ni moja ya Juhudi alizo ziunga Mkono wakati wa matembezi.

Pia amepongeza juhudi zinazofanywa na mradi wa fahari yetu Tanzania katika kukuza na kuendeleza utamaduni nyanda zajuu kusini na Tanzania.