Chuo kikuu cha Iringa kilifanya maadhimisho yake kwasiku mbili mfululizo tarehe 13.7 Na tarehe 14.7.2022. Maadhimisho hayo yalitanguliwa na maandamano yaliyoanza siku ya kwanza katika viwanja vya Chuo kikuu cha Iringa nakufika katika Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma, ambapo walimu, wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo walipokelewa na Makamu Mkuu wa chuo Prof. Ndelilio Urio katika Makumbusho, kisha kutembezwa  nakupewa masimulizi na wafanya kazi wa makumbusho.

Kilele cha siku ya chuo Kiuu cha Iringa kilitamatishwa siku ya pili katika viwanja vya chuo ambapo Mgeni rasmi wa maadhimisho alikuwa ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa. Adolf Mkenda pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa sambamba na wageni wengine.

Chuo kikuu cha Iringa ni moja kati ya wadau wakubwa wa makumbusho ya Mkoa Iringa kama ilivyo elezwa kwa undani kupitia tovuti yetu ya fahari yetu Tanzani.