Watafiti kutoka nchini Ujerumani kwa kushirikiana na mradi wa fahari yetu Tanzania ambao unasimamia makumbusho ya mkoa wa iringa (Iringa Boma ) walitembelea makabila mbalimbali wakati wakifanya utafiti wa zana tofauti zinazotumika katika makabila tofauti nchini Tanzania.

Jamii ya wamaasai katika eneo la Engaruka wilayani Monduli ,jijini Arusha kaskazini magharibi mwa Tanzania ni moja ya kabila ambalo lilifikiwa na watafiti hawa waliohitaji kujua na kujifunza kwa kina juu ya zana mbalimbali ambazo zilitumika kabla na hata baada ya ukoloni..

katika kufanikisha utafiti huo vijana wa jamii ya maasai walikuwa katika mstari wa mbele  kutoa ushirikiano wa karibu katika kufanikisha utafiti huo wenyedhumuni la kujua historia na asili ya zana mbalimbali za makabila tofauti ambazo ziliichukuliwa wakati wa ukoloni wa ujerumani .