Mwaka 2023 imetimu miaka  116  tangu kumalizika kwa vita vya majimaji vilivyodumu kuanzia mwaka 1905  hadi 1907 vikihusisha makabila mbalimbali kutoka kusini kwa Tanganyika walioungana chini ya kiongozi wao kinjekitile ngwale  kupinga utawala wa kikoloni wa kijerumani, katika mapigano hayo inakadiriwa Zaidi ya watu alfu 75 mpaka laki tatu walipoteza Maisha kutokana na njaa, magonjwa na unyanyasaji , huku askari kijerumani waliibuka washindi katika uwanja wa mapambano..

Kwa kutambua mchango wa wapambanaji waliopoteza Maisha katika vita hiyo wizara ya utalii Tanzania  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa utalii nchini waliandaa tamasha maalumu kwaajili ya maonesho ya sehemu mbalimbali nchini na mkoa wa Ruvuma ambapo Mgeni rasmi alikuwa naibu Waziri wa maliasilli na utalii Tanzania Mhe.Marry Masanja Pamoja nakuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na serikali.

Katika madhimisho hayo Mradi wa fahari yetu Tanzania na makumbusho ya mkoa Iringa Boma tulipata nafasi ya kushiriki katika maadhimisho ya miaka 116 tangu kumalizika kwa vita hiyo , kwa lengo la kujifunzana kudumisha ushirikiano na wadau mbalimbali wa utalii nchini Tanzania..