Maafsa wa Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma leo tume pata fursa ya kushiriki Washa ya kujijengea uwezo kuhusu mbinu za kufundisha chini ya mama yetu Dk.Kasumba kwa ajili ya programu ya kutembelea shule mbalimbali. Kaa tayari Makumbusho imekuandalia elimu toshelezi kwa ajili yako.

Wiki hii Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma tulipata ugeni wa Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Iringa (Waalimu watalajiwa) wenye lengo la kujifunza Historia ya Iringa na wakazi wake kwa ajili ya kuandika kazi mradi. Makumbusho imekuwa ni kituo cha kujifunza na kuelimisha kuhusu utamaduni wa watu mbalimbali. Tunakaribisha shule, vyuo na taasisi za kiserikali na zile binafsi kwa ajili ya kujifunza tamaduni na historia ya Iringa.

 

Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma imepata nafasi ya kushiriki kwenye uandaaji wa Makala ya redio ya Shirika la Utangazaji la Ujerumani kuhusu kumbukumbu ya Historia ya kikoloni nchini Tanzania kwa kuangazia namna gani wananchi wanaikumbuka na jitihada za taasisi hususan Makumbusho wanavyoitunza Historia hiyo.

Kulia ni Bwana, Jochen Rack kutoka Shirika la Utangazaji Ujerumani (Bavaria Broadcast Corporation)

Mnamo tarehe 5 mwezi wa 12, maonesho mapya yanayoelezea chimbuko na mabadiliko ya Binadamu yamefunguliwa rasmi na Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma. Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Tanzania na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa walihudhuria. Hafla ya ufunguzi iliambatana na burudani mpaka saa nne na nusu usiku.

Dkt. Augustine Philip Mahiga, Balozi na Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefariki dunia leo alfajiri 01 Mei, 2020 Jijini Dodoma.

Daima tutakumbuka na tutamenzi Dkt. Mahiga kama Balozi wa fahari yetu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kama Balozi wa Mkoa wa Iringa na watu wake kwa dunia nzima. Tangu alipofungua rasmi Makumbusho ya Mkoa wa Iringa Boma mwaka 2016, alitushauri na kutuongoza ktk kuendeleza kazi yetu na kuitangaza kitaifa na kimataifa. Tunamwombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi. Tunapenda kutoa salamu za rambirambi za dhati kwa familia na ndugu yake pamoja na watu wote walio karibu naye.