Maonesho ya Sanaa ya kukumbukwa

boma art exhibit boma art exhibit

Katika juma la ufunguzi wa Makumbusho ya Mkoa – Iringa Boma, tulimkaribisha mwanasanaa Hans Poppe, kutoka Canada ambaye familia yake ina asili ya Iringa. Michoro yake yenye ufanisi wa Kiswahili iliongeza thamani kubwa katika ufunguzi huu. Wanajamii walipata nafasi ya kukutana na msanii pamoja na matembezi katika Makumbusho. Miongoni mwa kazi hizi za sanaa zitaendelea kubaki katika Makumbusho.

Shukrani za dhati ziende kwa Hans na wote walioshiriki kukamilisha maonesho haya.

hans2 hans3

Picha na Darlene Parker na Hans Poppe

 

Makumbusho ya Mkoa – Iringa Boma yafunguliwa rasmi!!

Karibu kutembelea Makumbusho!

Kila siku Makumbusho itafunguliwa kuanzia saa 3:30 asubuhi mpaka saa 12:00.

Makumbusho inapatikana katikati mwa Mji wa Iringa. Hapa ni sehemu sahihi kwa ajili ya taarifa za nyakati tofauti za Hitoria ya Iringa, wakazi wake na tamaduni zao pamoja na sehemu za kusisimua zenye kuufanya upekee wa Iringa.

Irinaa Boma Museum
Karibu Makumbusho ya Mkoa – Iringa Boma

Pamoja na maonesho ya muda kuna taarifa za Historia ya Iringa na Tunu za Asili na Kitamaduni basi kuna cha kumvutia kila mmoja anayeweza kufika.

Grarama za kiingilio

Wakubwa – Wasio na Kibadli cha kuishi Nchini    – Shilingi 10,000

Wanafunzi – Wasion na Kibali cha kuishi Nchini   – Shilingi 5,000

Wageni wenye vibali vya kuishi Nchini                 – Shilingi 5,000

Watanzania Wakubwa                                          – Shilingi 3,000

Watanzania wanafunzi                                         – Shilingi 1,000

boma museum boma museum boma museum IMG_8007

Uzinduzi wa Iringa Boma-Makumbusho ya Mkoa na Kituo cha Utamaduni

Mwaka 2014, mradi wa fahari yetu ulianza kazi kubwa ya kukarabati Boma la wajerumani. Jengo hili liliachwa wazi na ofisi ya mkuu wa wilaya iliyokuwa ikilitumia kabla ya fahari yetu kuanza ukarabati. Moja ya malengo makuu ya mradi ni kutunza, kukuza, kutoa mwamko na kujivunia utamaduni. Kubadilishana na kushiriki kwa kuonesha masuala ya kitamaduni na kushirikisha umma.

Iringa Boma 2014
Boma prior to renovation in 2014

 

Baada ya kukamilika kwa ukarabati wa Boma, ambalo sasa ni makumbusho ya Mkoa na kituo cha utamaduni, siku ya Jumamosi Juni 25, 2016,  makumbusho yatafunguliwa kwa umma. Sherehe rasmi za ufunguzi zitafanyika siku hiyo kwa kushirikiana na wadau, wafuasi, washirika, wafadhili na wawakilishi wa serikali.

Iringa Boma 2016
The renovated Boma 2016

 

Ratiba kamili ya matukio ya siku hiyo itawekwa hapa katika wiki zijazo, hivyo tafadhali endelea kupitia tovuti yetu, lakini pia usisahau kuongeza tukio hili katika kalenda yako….It’s Iringa’s time to shine!

Karibuni! Tovuti yetu ipo hewani sasa.

Haikuwa rahisi. Ilihusisha majadiliano na kufikiri kwa muda mrefu, lakini hatimae tovuti ya fahari yetu ipo hewani. Live!

Tunawakaribisha ilikuweza kuchimba na kufahamu kuhusu Iringa, urithi na ütamaduni wake. Baadhi ya kurasa bado zinaendelea kufanyiwa marekebisho na maboresho ya hapa na pale. Tafadhali jisikie huru kutuma maoni yako kupitia anuani zetu.

Happy Browsing…