Mwaka 2014, mradi wa fahari yetu ulianza kazi kubwa ya kukarabati Boma la wajerumani. Jengo hili liliachwa wazi na ofisi ya mkuu wa wilaya iliyokuwa ikilitumia kabla ya fahari yetu kuanza ukarabati. Moja ya malengo makuu ya mradi ni kutunza, kukuza, kutoa mwamko na kujivunia utamaduni. Kubadilishana na kushiriki kwa kuonesha masuala ya kitamaduni na kushirikisha umma.

Iringa Boma 2014
Boma prior to renovation in 2014

 

Baada ya kukamilika kwa ukarabati wa Boma, ambalo sasa ni makumbusho ya Mkoa na kituo cha utamaduni, siku ya Jumamosi Juni 25, 2016,  makumbusho yatafunguliwa kwa umma. Sherehe rasmi za ufunguzi zitafanyika siku hiyo kwa kushirikiana na wadau, wafuasi, washirika, wafadhili na wawakilishi wa serikali.

Iringa Boma 2016
The renovated Boma 2016

 

Ratiba kamili ya matukio ya siku hiyo itawekwa hapa katika wiki zijazo, hivyo tafadhali endelea kupitia tovuti yetu, lakini pia usisahau kuongeza tukio hili katika kalenda yako….It’s Iringa’s time to shine!