Maombi ya masomo ya kubadilishana Muhula Ujerumani

Kwa Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Iringa!

Usikose nafasi hii nzuri ikiwa wewe ni mmoja wa walengwa wafuatayo:

Don’t miss this great opportunity if you belong the the following target groups:

  1. Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili ya Sanaa katika Utalii, Utamaduni na Jamii (Master of Arts in Tourism, Culture and Society – MATCS)
  2. Wafanyakazi wa Kiakademia kutoka idara ya Anthropolojia ya Utamaduni na Utalii na idara nyingine zenye utafiti ya kijamii na zilizo na utamaduni au nia ya kufundisha.

Fanya maombi kabla ya tarehe 21/11/2016 ili kushiriki muhula wa pili 2016/2017 katika Chuo cha Göttingen, Ujerumani

Angalia taarifa zote kuhusu kutuma maombi:

Nafasi hii inafadhiliwa na  Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kupitia Erasmus+ KA 107 (Mobility with Partner Countries): Go International Plus 2016 programme.

uoi_logo_modified_v2_uoi                                                                                                          ugoe-logo

 

Maonesho ya Sanaa ya kukumbukwa

boma art exhibit boma art exhibit

Katika juma la ufunguzi wa Makumbusho ya Mkoa – Iringa Boma, tulimkaribisha mwanasanaa Hans Poppe, kutoka Canada ambaye familia yake ina asili ya Iringa. Michoro yake yenye ufanisi wa Kiswahili iliongeza thamani kubwa katika ufunguzi huu. Wanajamii walipata nafasi ya kukutana na msanii pamoja na matembezi katika Makumbusho. Miongoni mwa kazi hizi za sanaa zitaendelea kubaki katika Makumbusho.

Shukrani za dhati ziende kwa Hans na wote walioshiriki kukamilisha maonesho haya.

hans2 hans3

Picha na Darlene Parker na Hans Poppe

 

Makumbusho ya Mkoa – Iringa Boma yafunguliwa rasmi!!

Karibu kutembelea Makumbusho!

Kila siku Makumbusho itafunguliwa kuanzia saa 3:30 asubuhi mpaka saa 12:00.

Makumbusho inapatikana katikati mwa Mji wa Iringa. Hapa ni sehemu sahihi kwa ajili ya taarifa za nyakati tofauti za Hitoria ya Iringa, wakazi wake na tamaduni zao pamoja na sehemu za kusisimua zenye kuufanya upekee wa Iringa.

Irinaa Boma Museum
Karibu Makumbusho ya Mkoa – Iringa Boma

Pamoja na maonesho ya muda kuna taarifa za Historia ya Iringa na Tunu za Asili na Kitamaduni basi kuna cha kumvutia kila mmoja anayeweza kufika.

Grarama za kiingilio

Wakubwa – Wasio na Kibadli cha kuishi Nchini    – Shilingi 10,000

Wanafunzi – Wasion na Kibali cha kuishi Nchini   – Shilingi 5,000

Wageni wenye vibali vya kuishi Nchini                 – Shilingi 5,000

Watanzania Wakubwa                                          – Shilingi 3,000

Watanzania wanafunzi                                         – Shilingi 1,000

boma museum boma museum boma museum IMG_8007