Maonesho ya siku ya Sabasaba (77) Mkwawa

 

Makumbusho ya mkoa Iringa Boma na Mradi wa fahari yetu Tanzania tulipata nafasi ya kushiriki katika maonesho ya sababa yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo kikuu kishiriki cha Dar es laam Mkwawa, Maonesho hayo yalifunguliwa na Mgeni rasmi Mh.Saad Mtambule Mkuu wa wilaya ya Mufindi Iringa.

Banda la makumbusho ya mkoa Iringa Boma tulipata nafasi ya kutembelewa na Mgeni rasmi wa maonesho haya yaliyofanyika siku ya sabasaba kamailivyo fanyika kwa mabanda mengine, Kutangaza vivutio vya ndani na historia yetu kama watanzania ni moja kati ya vitu alivyo sisitiza mgeni rasmi katika maonesho haya pindi alipo tembelea banda letu.

“Watu wengi wanajua kuwa utalii ni kwenda Mbugani au kupanda mlima Kilimanjaro na kufika katika maeneo ya fukwe, hapana utalii ni Zaidi ya hivi Iringa boma nimependa juhudi zenu katika kutanga utalii wa malekale na historia  lakini tusiishie hap ana tuongeze kasi katika kutangaza utalii huu duniani kote”.

Sikukuu ya sababa illianza rasmi mwaka 1954 tarehe 7 ya mwezi wa 7 baada ya chama cha   TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION (TAA) na AFRICAN ASSOCIATION (AA) kuungana na kupatikana chama cha TANGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION  (TANU), chama ambacho kili saidia katika kudai uhuru wa Nchi yaTanganyika (1960) chini ya mwalimu Nyerere rais wa kwanza wa Tanganyika.

Kwa kuwa sera ya chama hiki ilikuwa ni Kilimo “Kilimo nii utii wa Mgongo” basi watu wengi waliamua kujihusisha na shughuli za kilimo na walipeleka mazao yao kila siku katika maonesho  yakikuwa yakifanyika siku ya tarehe 7 Mwezi wa 7 ilikuenzi muungano huo, kwa hivi sasa sikuku hii ya wakulima imegeuka na kuwa kama siku ya wafanyabiashara.

Ukumbi wa Siasa ni Kilimo ulipo Iringa mjini ni moja kati ya mazao ya sera ya kilimo iliyoanzishwa miaka ya 1954 baada ya kuzaliwa kwa chama cha TANU.

 

 

 

 

Matembezi ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa

Wakati kaitka picha ni Mkurugenzi wa makumbusho ya Taifa Dr. Noel Lwoga alipata nafasi ya kutembelea Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma wakatiakipita Iringa kuelekea Dodoma. Uhifadhi wa malikale kama sehemu ya makumbusho na kituo cha utamaduni na  Masimulizi / historia za wenyeji na Machifu kwa wageni hata wazawa wa Mkoa wa Iringa ni moja ya Juhudi alizo ziunga Mkono wakati wa matembezi.

Pia amepongeza juhudi zinazofanywa na mradi wa fahari yetu Tanzania katika kukuza na kuendeleza utamaduni nyanda zajuu kusini na Tanzania.

 

Iringa Boma Easter Market Event

Ni takribani miaka mi tatu ilipita bila kufanikisha tukio la Easter market katika viwanja vya makumbusho, sababu kubwa ilikuwa Ni ugonjwa wa Uviko 19 uliopelekea kupigwamarufuku kwa mikusanjiko ya watu, mikutano na shughuli mbalimbali zenyeuhitaji wa watu wengi.

Mwaka 2022 umekuwa mwaka wenye bahati kwakufanikiwa kufanya Event hii iliombatana na uzinduzi wa mgahawa wetu Aroma Coffee House @boma, licha ya tukio kupita lakini Mgahawa umeanza kufanya kazi rasmi.

Uongozi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma unatoa shukrani zake za dhati kwa wote walio fanikisha kufanyika kwa tukio hili na wale walio hudhulia siku ya tukio. Uongozi wa mradi unawakaribisha tena kwenye matukio mengine yatakayokuwa yanaendelea, kwani mwisho wa tukio moja ndio mwanzo wa matukio mengine.

Utafiti Mkoa wa Mtwara

Hapo zamani mfumo wa utawala wa kikoloni uliigawa Tanganyika (Tanzania) kwenye majimbo makubwa nane (8), Jimbo la Kusini ambalo lilijumuisha Mikoa ya Ruvuma,Lindi, na Mtwara amabapo makao makuu yalikuwa lindi.

Mwaka 1971 ndipo ulipo anzishwa Mkoa wa Mtwara, kuanzishwa kwa  Mkoa huu kulitokakana na mpango wa Madaraka Mikoani ulio simamiwa na Rais wakwanza wa Tanzania Mwl.Julius.K. Nyerere uliokuwa na lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.Tafsiri ya neno “NTWARA” ambalo kwasasa ni Mtwara linatokana na neno la kimakonde “kutwara” lenye maana ya ku-twaaliwa (kuvamiwa na kuchukuliwa mateka).

Asilimia 75 ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara ni Wamakonde.  Wayao na Wamakua miongoni mwa makabila yanayo patikana katika mkoa huu. Mradi fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma tulifanikiwa kufika Mtwara kwa lengo la utafiti, Mikindani,Mtwara mjini, Tandahimba na Newala ni baadhi ya maeneo tuliofanikiwa kufika wakati wautafiti.

Utafiti Mkoa wa Lindi

Lindi Ni miongoni mwa mikoa inayopatikana Tanzania ni moja kati ya Mikoa mikongwe ilioanza kati ya karne ya 11 kwenye historia ya Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Historia ya Mkoa wa Lindi inapambwa na badhii ya maeneo yaliopo kwenye wilaya za Mkoa huo. Jina la Lindi maana yake ni SHIMO REFU, Bandari ya Lindi ilitumika katika kusafirishia watumwa kutoka Ziwa Nyasa. Waarabu waliofika karne ya 18, wahindi,wajerumani na waingereza ni miongoni mwa mataifa yaliyofanikiwa kuishi katika mkoa huu.

Mradii wa fahari yetu Tanzania na makumbusho ya Mkoa Iringa Boma tulifanikiwa kufika katika mkoa wa Lindi kwa ajili ya utafititi wa mambo kale na zana za asili zilizo tumika na wazawa tangu miaka 100 iliyopita. Lindi mjini, Kilwa Kipatimu (Nandete), Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani Songo Mnara (Mji wa kale wa kiaarabu), Kilwa Masoko na Nchinga ni baadhi ya maeneo tuliyofanikiwa kuetembelea na kufanya utafiti katika mkoa wa Lindi.