“Karibuni sana wageni kuwekeza katika Utalii wa Tanzania, inawezekana ukawekeza katika utalii wa chakula, utalii wa kiutamaduni lakini pia utalii wakupokea wageni majumbani (Home Stay Tourism) Lengo letu ni kuhakikisha tuna kuza na kutangaza utalii wa Tanzania kwa njia yoyote ile” Mhe. Angela Kairuki Waziri wa maliasili na Utalii Tanzania. ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Swahili International Expro yaliyofanyika jijini Dar es laam.
Mr.Jimson sanaga Meneja mwenza mradi wa fahari yetu Tanzania na makumbusho ya mkoa Iringa boma anasema ni mara yao ya nne sasa kuhudhuria katika maonesho hayo makubwa ya utalii Tanzania, na kila mwaka maonesho hayoyamekuwa yakiutofauti.
“Kwa miaka yote minne ambayo tumehudhuria katika maonesho haya tumeona utofauti mkubwa sana, maonesho yametusaidia katika kutangaza utalii wetu wa Tanzania na hususa ni utalii wa nyanda za juu kusini” hata hivyo bado tunanafasi kubwa sana yakuendelea kutangaza utaklii wandani na hata wakuhistoria ameongeza Mr. Sanga yakuwa mradi wafahari yetu kwasasa upo kwenye utafiti wa masimulizi ya kale yaliyo hatiani kupotea kwa lengo la kuyakusanya na kuyahifadhi kwa jili ya vizazi vijavyo.
Maonesho ya Swahili International Tourism Expro (S!TE) hufanyika kila mwaka nchini Tanzania, maonesho haya yanalengo la kukutanisha wadau mbalimbali wa utalii wandani ya nchi na nnje ya nchi kwalengo la . Kwamwaka wa 2023 maonesho haya yamefanyika kuanzania tarehe 6 hadi mwezi wa 10 katika viwanja wa mlimani City jijini Dar es Laam.
Je! unatafuta eneo sahihi kwa ajili ya kufanya biashara ya Mgahawa, ndio pengine hujui wapi panaweza kuwa eneo sahihi zaidi, acha nikufahamishe yakuwa Makumbusho ya mkoa Iringa Boma inakutangazia kuwa inapangisha eneo lake la mgahawa kwa Muwekezaji aliye tayari.
Kuna kila sababu za kuwekeza katika eneo hili .
1.Eneo lipo katikati ya mji wa Iringa (Iringa Boma ) ilipokuwa ofisi ya mkuu wa Wilaya.
2. Nisehemu nzuri yenye muingiliano wa wageni kutoka nchi mbalimbali kutokana uwepo wa Makumbusho ya Mkoa.
3. Ulinzi na usalama ni wa hali ya juu.
Unasubiri nini sasa kwa mawasiliano zaidi tupigie kupitia
+255 753 975 333
+255 762 424 642
Sikukuu ya Sabasaba, inayojulikana pia kama Saba Saba Day, ni sikukuu ya kitaifa nchini Tanzania inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 7 Julai.
Sikukuu ya Sabasaba imekuwa muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano wa Watanzania na kuadhimisha historia ya taifa. Pia, inatoa fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kuonyesha bidhaa na huduma zao na kujenga uhusiano na wateja wapya.
Kwa mkoa wa Iringa sikukuu hii inaadhimishwa katika kijiji cha Pawaga ambapo mradi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma wamedhamini Mashindano ya ngoma za Asili na kutoa zawadi za jezi kwa washiriki waliyofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali katikla michuano ya sababa.
Akizungumza na wananchi Mkuu wa wilaya wa Iringa amabaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa wiki ya sabasaba anasema watu wengi wanasahau asili yao kutokana na mabadiliko ya kiutandawazi hivyo amepongeza juhudi zinazofanywa na mradi wa fahari yetu Tanzania katika kuendeleza na kuenzi utamaduni kwakudhamini mashindano hayo.
Naye mkurugenzi mradi wa fahari yetu Tanzania Dr.Jan Kuever ameeleza kuwa mradi wa fahari yetu umekuwa ukijihusisha na kukuza,kutangaza na kuendeleza shughuli za kiutamaduni tangu kuanzishwa kwake.
Njombe ni moja kati ya mikoa inayopatikana nyanda za juu kusini mwa Tanzania, awali mkoa wa Njombe uliungana na Mkaoa wa Iringa na kufahamika kama mkoa mmoja wa Iringa hadi serikali ilipoamua kutenganisha mikoa hii na kila mmoja kujtegemea kisiasa. Kama ilivyo katika mikoa mingine nchini Tanzania mkoa wa njombe ni moja kati ya mkoa wenye makabila kama Wabena, Kinga na wapangwa.
Njombe ni miongoni mwa mikoa iliyobarikiwa kuwa na historia kubwa Tangu kipindi cha ukoloni na umisionary. Kabila la wabena ni miongoni mwa makabila yaliyo husika kwenye vita ya majiji iliyopigwana mwaka 1905-1907, Huku Njombe ikitiumika akama sehemu ya kumaliza vita hivto katika eneo la sawala.
“Wajerumani waliwaalika viongozi wote wa Vita ya Maji na kuwachimbisha shimo kwa lengo la kuamaliza vita hiyo mara ya kwanza waliwapa mavazi baada ya kuchimba, lakinia mara ya pili mamabo yalikuwa ndivyo sivyo kwani viongozi wa makabila waldhani watapewa nguo tena badala yake waliuliwa kikatili katika eneo hili” anaeleaza Mzee William mkazii wa Sawala.
Mradi wa Fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa BOMA kwa kushirikiana na makumbusho nyingine zilizopo Ujerumani wapo kwenye tafiti zinazohusisha historia za mbalimbali Tangu kipindi cha ukoloni na ujio wa missionary Afrika, sambamba na kuangalia baadhi ya vitu vilivyo chukuliwa na wageni wa kijerumani ambavyo hadi sasa vipo nchini kwao pasi nakujua vilikuwa na maana gani na matumizi gani.
Mwaka 2023 imetimu miaka 116 tangu kumalizika kwa vita vya majimaji vilivyodumu kuanzia mwaka 1905 hadi 1907 vikihusisha makabila mbalimbali kutoka kusini kwa Tanganyika walioungana chini ya kiongozi wao kinjekitile ngwale kupinga utawala wa kikoloni wa kijerumani, katika mapigano hayo inakadiriwa Zaidi ya watu alfu 75 mpaka laki tatu walipoteza Maisha kutokana na njaa, magonjwa na unyanyasaji , huku askari kijerumani waliibuka washindi katika uwanja wa mapambano..
Kwa kutambua mchango wa wapambanaji waliopoteza Maisha katika vita hiyo wizara ya utalii Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa utalii nchini waliandaa tamasha maalumu kwaajili ya maonesho ya sehemu mbalimbali nchini na mkoa wa Ruvuma ambapo Mgeni rasmi alikuwa naibu Waziri wa maliasilli na utalii Tanzania Mhe.Marry Masanja Pamoja nakuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na serikali.
Katika madhimisho hayo Mradi wa fahari yetu Tanzania na makumbusho ya mkoa Iringa Boma tulipata nafasi ya kushiriki katika maadhimisho ya miaka 116 tangu kumalizika kwa vita hiyo , kwa lengo la kujifunzana kudumisha ushirikiano na wadau mbalimbali wa utalii nchini Tanzania..