Moja kati ya mambo muhimu ya kuimarisha mradi na kuufanya kuwa endelevu ni kuendeleza na kuwa na utaalam wa kutosha wa ndani. Kutokana na hilo mradi unajenga uwezo katika maeneo ya usimamizi fanisi, kubuni shughuli na kuzitekeleza, utaalam wa kitaaluma na ujuzi katika ujasiriamali.