“Karibuni sana wageni kuwekeza katika Utalii wa Tanzania, inawezekana ukawekeza katika utalii wa chakula, utalii wa kiutamaduni lakini pia utalii wakupokea wageni majumbani (Home Stay Tourism) Lengo letu ni kuhakikisha tuna kuza na kutangaza utalii wa Tanzania kwa njia yoyote ile” Mhe. Angela Kairuki Waziri wa maliasili na Utalii Tanzania. ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Swahili International Expro yaliyofanyika jijini Dar es laam.

Mr.Jimson sanaga Meneja mwenza mradi wa fahari yetu Tanzania na makumbusho ya mkoa Iringa boma anasema ni mara yao ya nne sasa kuhudhuria katika maonesho hayo makubwa ya utalii Tanzania, na kila mwaka maonesho hayoyamekuwa yakiutofauti.

“Kwa miaka yote minne ambayo tumehudhuria katika maonesho haya tumeona utofauti mkubwa sana, maonesho yametusaidia katika kutangaza utalii wetu wa Tanzania na hususa ni utalii wa nyanda za juu kusini” hata hivyo bado tunanafasi kubwa sana yakuendelea kutangaza utaklii wandani na hata wakuhistoria ameongeza Mr. Sanga yakuwa mradi wafahari yetu kwasasa upo kwenye utafiti wa masimulizi ya kale yaliyo hatiani kupotea kwa lengo la kuyakusanya na kuyahifadhi kwa jili ya vizazi vijavyo.

Maonesho ya Swahili International Tourism Expro (S!TE) hufanyika kila mwaka nchini Tanzania, maonesho haya yanalengo la kukutanisha wadau mbalimbali wa utalii wandani ya nchi na nnje ya nchi kwalengo la . Kwamwaka wa 2023 maonesho haya yamefanyika kuanzania tarehe 6 hadi mwezi wa 10 katika viwanja wa mlimani City jijini Dar es Laam.