Dkt. Jan Kuever
Mkurugenzi Mtendaji
Tangu kufuzu masomo yake ya Shahada ya Uzamili (M.A) katika masuala ya Anthropolojia na Utamaduni nchini Ujerumani mwaka 2007, Dkt. Jan Kuever anafanya kazi ya uhadhiri na pia katika upande wa utawala katika chuo kikuu cha Iringa.
Yeye ni mwandishi na mwanzilishi wa mradi wa fahari yetu na pia ndiye meneja wa Mradi ambaye anajukumu la kusimamia na kuratibu shughuli zote zinazohusu mradi.
Dkt. Kuever pia alitumia mradi wa fahari yetu kama uchunguzi kifani (case study) katika utafiti kwa masomo yake ya Shahada ya Uzamivu (PhD) ya masuala ya Urithi na Utamaduni katika chuo kikuu cha BTU Cottbus-Senftenberg, nchini Ujerumani. Utafiti alioufanya unachunguza kinadharia na vitendo uhusiano kati ya utamaduni,urithi na maendeleo endelevu.
Deonis Mgumba
Mhifadhi Makumbusho
Deonis alimaliza Shahada ya Uzamili ya Sanaa katika Utamaduni na Jamii ya Utalii, Chuo Kikuu cha Iringa mwaka 2016.
Kwasasa anafanya kazi kama msimamizi (mhifadhi) wa Makumbusho ya Mkoa na Kituo cha Utamaduni Iringa Boma. Pia anasaidia utafiti wa makumbusho ili kuifikia jamii na anatumia utaalamu wake kama mwongoza wa watalii katika makumbusho ya Mkoa.
Imran Daud
Afsa uhamasishaji Jamii
Imran alihitimu shahada ya Utamaduni Anthropolojia na Utalii katika Chuo Kikuu cha Iringa mwaka 2018.
Kwasasa anaendelea na masomo yake ya Shahada ya Uzamili ya Maendeleo ya Jamii na Mipango ya Miradi katika Chuo Kikuu cha Iringa.
Imran alijiunga na Makumbusho ya Mkoa- Iringa Boma kama mtu wa kujitolea, mwongozo wa watalii, mpiga picha, na mratibu wa hafla mnamo mwaka 2019. Kwa sasa ameajiriwa kama Afisa Uhamasishaji Jamii.
Jimson S. Sanga
Meneja Msaidizi
Jimson Sanga ni Mhadhiri katika idara ya Anthropolojia, utamaduni na utalii katika chuo kikuu cha Iringa tangu mwaka 2011. Mwaka 2014, alihitimu Shahada ya Uzamili (M.A) ya Utalii, Utamaduni na Jamii.
Sanga anajukumu la kumsaidia Meneja Mradi katika kuratibu na kufatilia masuala yote yanayohusu mradi ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu na kuendeleza shughuli na mawasiliano yote yanayohusu mradi.
Akihusianisha na historia ya utafiti wake alioufanya katika masuala ya Ethnolojia na muziki (Ethnomusicology) moja ya shabaha kuu ya kazi yake ni kufanya muziki na ngoma za asili kuwa bidhaa za kibiashara na zenye faida kupitia utalii.
Virginia Vangayena
Mhudumu Mapokezi
Virginia Vangayena alihitimu elimu ya cheti cha kazi ya kuongoza watalii katika Chuo cha Taifa cha Utalii mwaka 2010. Pia alipata Diploma ya Mafunzo ya Burudani na utalii katika Chuo Kikuu cha Iringa mwaka 2021.
Mwaka 2017 alianza kujitolea katika Makumbusho ya Iringa Boma, na sasa ameajiriwa kama mhudumu wa mapokezi na mwongoza wageni.
Virginia anaendelea na masomo yake ya shahada ya kwanza ya anthropolojia ya kitamaduni na utalii katika Chuo Kikuu cha Iringa.