Maarifa yenye kuaminika ya masuala ya urithi na rasilimali za utamaduni katika mkoa wa Iringa ni suala muhimu kwa mikakati ya maendeleo endelevu.
fahari yetu inapanua maarifa hayo kwa kukusanya na kuandaa taarifa kuhusu maeneo ya kitamaduni na namna unavyotekelezwa, na pia kutathmini mahusiano na mitazamo ya watu juu ya urithi wao.