Utafiti wa mradi huu unachunguza uhusiano kati ya utamaduni na uzalishaji wa kiuchumi katika mkoa wa Iringa. Utafiti unatathmini mikakati ya jadi ya kujikimu kama vielelezo vya utamaduni na kuchunguza njia mpya za kutumia utamaduni kama njia ya kujiongezea kipato kama vile kupitia ujasiriamali wa mambo ya kitamaduni na utalii.