Mkoa wa Iringa umejaa maajabu ya utamaduni na anuai asilia vinavyofaa kwa talili. Chumba hiki ni kwaajili ya kujifunza kuhusu maeneo mbalimbali ya kutembelea baada ya kuondoka Makumbusho:

  •   Gundua maeneo ya akiolojia yenye zana za mawe na michoro ya kale.
  •   Fuatilia nyayo za Chief Mkwawa na kuelewa kikamilifu historia ya Wahehe na           upinzani wao dhidi ya uvamizi wa kikoloni.
  •   Jifunze kuhusu ukuaji wa mji wa Iringa kutoka zama za kikoloni, harakati za uhuru     hadi sasa.
  •   Furahia mazingira mazuri na wanyamapori wanaopatikana Kusini mwa Tanzania       kwa kufanya ziara ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.