Mkoa wa Iringa umejaa maajabu ya utamaduni na anuai asilia vinavyofaa kwa talili. Chumba hiki ni kwaajili ya kujifunza kuhusu maeneo mbalimbali ya kutembelea baada ya kuondoka Makumbusho:
- Gundua maeneo ya akiolojia yenye zana za mawe na michoro ya kale.
- Fuatilia nyayo za Chief Mkwawa na kuelewa kikamilifu historia ya Wahehe na upinzani wao dhidi ya uvamizi wa kikoloni.
- Jifunze kuhusu ukuaji wa mji wa Iringa kutoka zama za kikoloni, harakati za uhuru hadi sasa.
- Furahia mazingira mazuri na wanyamapori wanaopatikana Kusini mwa Tanzania kwa kufanya ziara ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.