Iringa Boma pia hutoa taarifa kuhusu na kufanya ziara katika vivutio vingine vya utalii vilivyoendelezwa na mradi wa fahari yetu:
- Ziara ya utalii Iringa mjini: Fuata nyayo za historia ya mji wa Iringa
- Mwamba wa Gangilonga: Jabali linaloongea
- Michoro ya mwamba Igeleke: Mandhari na sanaa katika mwamba mkongwe
- Mnara wa kumbukumbu Kitanzini: Kumbukumbu ya ukandamizaji wa mkoloni
- Mnara wa kumbukumbu Lugalo: Uwanja wa vita aliposhindwa Mjerumani
- Ngome na Makumbusho ya Kalenga: Makao makuu ya Chifu Mkwawa
- Mlambalasi: Eneo la Maficho ya mwisho ya Mkwawa na kaburi lake
- Eneo la Mali Kale Isimila: Machimbo ya akiolojia na nguzo za asili.