Kituo cha Utamaduni na Utalii cha Mkwawa ni kituo kipya kinachojengwa na fahari yetu kwa ubia na halmashauri ya wilaya ya Iringa. Kituo hiki kipo kilomita 40 kutoka Iringa mjini,  kando kando ya barabara inayoelekea mbuga ya Taifa ya Ruaha, karibu na kituo cha historia cha Mlambalasi na lilipo kaburi la chifu Mkwawa. Kituo hiki kitakuwa ni mahali pa kupumzikia kwa wanaofanya utalii wa wanyamapori, lakini pia ni sehemu salama na faragha kwa kufanyia mazungumzo, mikutano au warsha  kwa makampuni, taasisi au miradi. Sehemu hii pia inafaa kwa mapumziko binafsi ya mwisho wa wiki, kwa wanaopenda kufanya mapumziko nje ya mji. Mbali na shughuli nyingine, kituo hiki kinatarajia kutoa huduma zifuatazo:

 • Maonesho madogo ya maliasili na urithi wa utamaduni
 • Huduma za taarifa kuhusu Iringa kwa watalii
 • Ziara / Kutembelea eneo la kihistoria la Mlambalasi/ Kaburi la Mkwawa.
 • Ziara/ Kuona maisha ya wenyeji (Kijiji cha Wamasai, Shughuli za kilimo, Maeneo ya Ibada)
 • Vyakula na Vinywaji
 • Huduma za Choo
 • Kambi / malazi
 • Muziki wa Utamaduni / Maonesho ya Ngoma
 • Huduma za Internet / Huduma za Steshenari
 • Kuonesha na kuuza bidhaa za utamaduni
 • Huduma za mikutano
 • Uchomaji nyama kitamaduni
 • Kituo cha jamii cha utafiti