Chumba hiki ni kwaajili ya kuhifadhi na kuhuisha urithi wa utamaduni wa Iringa katika kila nyanja. Vitu vyote vilivyooneshwa humu ndani vimechangiwa na watu wanaoishi katika Mkoa wa Iringa. Vifaa hivi vimetolewa katika vijiji, makabila na jamii mbalimbali za Iringa. Na vingi vyao vina mahusiano na njia za jadi na mifumo ya maisha ambayo yanaanza kutoweka.
Hapa utajifunza zaidi kuhusu njia za jadi za uvunaji, kuhifadhi, kuandaa na kula chakula cha asili Iringa. Vifaa vilivyooneshwa vitakusimulia pia hadithi kuhusu muziki, ngoma, ibada, usafiri, biashara na mafunzo mengine mengi.