Katika chumba hiki utakutana na maonesho ya kusisimua ambayo hutoa ufahamu wa aina mbalimbali katika maisha ya utamaduni na mazingira ya Nyanda za Juu Kusini.

Maonesho ya kwanza katika chumba hiki ni kuhusu kazi ya waganga wa jadi mkoani Iringa. Hadi leo waganga wa jadi wanashika nafasi muhimu katika jamii na dhana zao za kiafya, kiroho, imani, na ibada. Picha na zana za maonyesho hayo zinaonesha kazi zao na jinsi wanavyoweza kusaidia maisha ya watu.