Sikukuu ya Sabasaba, inayojulikana pia kama Saba Saba Day, ni sikukuu ya kitaifa nchini Tanzania inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 7 Julai.

Sikukuu ya Sabasaba imekuwa muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano wa Watanzania na kuadhimisha historia ya taifa. Pia, inatoa fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kuonyesha bidhaa na huduma zao na kujenga uhusiano na wateja wapya.

Kwa mkoa wa Iringa sikukuu hii inaadhimishwa katika kijiji cha Pawaga ambapo mradi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma wamedhamini Mashindano ya ngoma za Asili na kutoa zawadi za jezi kwa washiriki waliyofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali katikla michuano ya sababa.

Akizungumza na wananchi Mkuu wa wilaya wa Iringa amabaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa wiki ya sabasaba anasema watu wengi wanasahau asili yao kutokana na mabadiliko ya kiutandawazi hivyo amepongeza juhudi zinazofanywa na mradi wa fahari yetu Tanzania katika kuendeleza na kuenzi utamaduni kwakudhamini mashindano hayo.

Naye mkurugenzi mradi wa fahari yetu Tanzania Dr.Jan Kuever ameeleza kuwa mradi wa fahari yetu umekuwa ukijihusisha na kukuza,kutangaza na kuendeleza shughuli za kiutamaduni tangu kuanzishwa kwake.