Njombe ni moja kati ya mikoa inayopatikana nyanda za juu kusini mwa Tanzania, awali  mkoa wa Njombe  uliungana na Mkaoa wa Iringa na kufahamika kama mkoa mmoja wa Iringa hadi serikali ilipoamua kutenganisha mikoa hii na kila mmoja kujtegemea kisiasa. Kama ilivyo katika mikoa mingine nchini Tanzania mkoa wa njombe ni moja kati ya mkoa wenye makabila kama Wabena, Kinga na wapangwa.

Njombe ni miongoni mwa mikoa iliyobarikiwa kuwa na historia kubwa Tangu kipindi cha ukoloni na umisionary. Kabila la wabena ni miongoni mwa makabila yaliyo husika kwenye vita ya majiji iliyopigwana mwaka  1905-1907, Huku Njombe ikitiumika akama sehemu ya kumaliza vita hivto katika eneo la sawala.

“Wajerumani waliwaalika viongozi wote wa Vita ya Maji na kuwachimbisha shimo kwa lengo la kuamaliza vita hiyo mara ya kwanza waliwapa mavazi baada ya kuchimba, lakinia mara ya  pili mamabo yalikuwa ndivyo sivyo kwani viongozi wa makabila waldhani watapewa nguo tena badala yake waliuliwa kikatili katika eneo hili” anaeleaza Mzee  William  mkazii wa Sawala.

Mradi wa Fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa BOMA kwa kushirikiana na makumbusho nyingine zilizopo Ujerumani wapo kwenye tafiti zinazohusisha historia za mbalimbali Tangu kipindi cha ukoloni na ujio wa missionary Afrika, sambamba na kuangalia baadhi ya vitu vilivyo chukuliwa na wageni wa kijerumani ambavyo hadi sasa vipo nchini kwao pasi nakujua vilikuwa na maana gani na matumizi gani.