Chuo Kikuu cha Göttingen, Ujerumani
www.uni-goettingen.de/en
Fahari yetu inashirikiana na Taasisi ya Ethnolojia pamoja na kituo cha utafiti wa masuala ya jamii kilicho ndani ya chuo hiki cha serikali cha ujerumani. Ushirikiano kati ya fahari yetu na Chuo Kikuu cha Göttingen unasaidia katika kukuza taaluma katika masuala ya urithi wa utamaduni na vilevile kujiongezea uwezo na sifa kupitia semina za kimataifa, kubadilishana walimu, na kwa pamoja kufanya tafiti na maonesho mbalimbali.
Shirika la ACRA
www.acra.it
Ni shirika lisilo la kiserikali la kimataifa lenye lengo la kuondoa umasikini katika makundi yaliyotengwa kwa kutumia njia mbalimbali za uvumbuzi na ufumbuzi wa pamoja. Shirika linashiriki katika kubuni na kutekeleza mipango ya kuendeleza utalii ilikunufaisha watu masikini. ACRA inashiriki pia katika ukarabati wa majengo ya kihistoria.
Shirika la Kuendeleza Watoto
www.envaya.org/ccdo
Children Care Development Organisation (CCDO) ni shirika lisilo la kiserikali. Linasaidia mradi katika kuendeleza na kutekeleza programu za mafunzo kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kutoa utaalam wa mbinu za uhamasishaji na uwezeshaji jamii. Kwa mfano, shirika linashiriki katika kuunda makundi ya sanaa, kuanzisha na kuendesha mikopo midogo.
Shirika la Uhifadhi wa Wanyamapori
www.wcs.org / www.wcstanzania.org
Shirika hili la kimataifa lisilo la kiserikali linausaidia mradi kwa kuchangia katika masuala ya taaluma na uzoefu wa uhifadhi wa viumbe hai, ushiriki, ukamilishi na usimamizi wa rasilimali za utamaduni. Shirika pia linaendeleza na kutekeleza programu mbalimbali za mafunzo kwa jamii.
Mkoa wa Iringa
www.iringa.go.tz / www.pmoralg.go.tz
Mkoa, kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inatoa msaada wa kiutawala, na pia ni kiungo kati ya serikali kuu na serikali za mitaa. Chombo hiki pia kinachukua jukumu katika kufanikisha ushirikiano kati ya mradi na umma na kutoa misaada ya kiutawala kama vile kuwezesha kufikika kwa maeneo yaliyo katika mradi,kutoa vibali na maeneo kwa ajili ya mradi, kusaidia mradi na vizuizi vya kisiasa, kuandaa matamasha na matukio mengine ya utamaduni
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa
www.iringadc.go.tz
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inausaidia mradi katika kuendeleza utekelezaji wa uhamasishaji jamii, kuanzisha na kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali vijijini katika Mkoa wa Iringa .
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
www.iringamunicipalcouncil.go.tz
Ikiwa ni mwenyeji wa mradi, ofisi ya Halmashauri ina nafasi na wajibu mkubwa katika kuhamasisha jamii iliyopo katika Manispaa kuthamini, kutunza, kuendeleza, na kuendelea kutangaza kwa watalii maeneo lengwa ya kiutamaduni.
Makumbusho ya Taifa / Nyumba ya Utamaduni
www.houseofculture.or.tz
Makumbusho ya Taifa ni mdau wa makumbusho mbalimbali za Tanzania yenye lengo la kuhifadhi na kuonesha historia na mazingira asilia ya Tanzania. Makumbusho ya Taifa yanausaidia mradi kwa kutoa utaalam na uzoefu wake katika kurejesha upya maeneo ya kitamaduni na maonesho.
Washirika
Mradi wa SPANEST
www.tanzaniaparks.com/news/news_SPANEST.html
www.facebook.com/southerncircuitproject
Ni programu inayofadhiliwa na Hifadhi za Taifa Tanzania na Umoja wa Mataifa ili kuhifadhi viumbehai na kusimamia maliasili katika maeneo yanayozunguka hifadhi za Taifa katika Nyanda za Juu Kusini. SPANEST inachangia uzoefu wa kuhamasisha wananchi kutafuta njia mbadala ya kujiingizia kipato kupitia utamaduni na utalii. Shirika pia linatoa utaalam wa masuala ya uchoraji man dhari.
Wizara ya Maliasili na Utalii
www.mnrt.go.tz
Idara ya Utalii na Idara ya Mambo Kale: Vyombo hivi vya serikali vinauongezea nguvu mradi kwa kusaidia utaalam wa uhifadhi na urejeshaji wa maeneo ya kihistoria (Idara ya Mambo Kale), na kutengeneza, kusimamia na kutekeleza sera ya utalii na urithi wa utamaduni (Idara ya Utalii).
Hifadhi ya Taifa Tanzania
www.tanzaniaparks.com
Chombo hiki kinauchangia mradi utaalam wake katika kukuza utamaduni na masoko ya utalii.
Bodi ya Utalii Tanzania
www.tanzaniatouristboard.com
Chombo hiki pia kinachangia utaalam katika kukuza utamaduni na masoko ya utalii kwa mradi.