Jamii inayozunguka maeneo ya utamaduni,ya hifadhi na mkoa kwa ujumla inahamasishwa kikamilifu juu ya uwezo na umuhimu wa utamaduni na urithi na kuhusishwa pia katika utambulisho wa rasilimali za urithi wa utamaduni katika mazingira yao. Ili kuwawezesha watu kutumia rasilimali hizo kwa ajili ya kuboresha vipato vyao, mafunzo yenye kulenga kuleta matokeo thabiti yanafanyika katika maeneo yafuatayo:
- Urithi wa utamaduni na usimamizi wa Maliasili
- Utamaduni na ujuzi wa biashara ya utalii na ujasiriamali
- Ujuzi wa kuongoza watalii
- Ukarimu na huduma kwa wateja