fahari yetu chini ya chuo kikuu cha Iringa (UoI) inafanya mabadilishano ya kitaaluma na ushirikiano na vyuo vikuu mbalimbali vya kimataifa katika nyanja zifuatazo:
- Kubadilishana wanafunzi pamoja na walimu wataalam na taasisi ya Ethnolojia katika Chuo Kikuu cha Goettingen, nchini Ujerumani.
- Kuwa na shule / Kozi ya pamoja ya majira ya joto na kufanya tafiti za pamoja na chuo kikuu cha Brandenburg Technical Cottbus-Senftenberg, cha nchini Ujerumani kupitia kitengo chake cha mafunzo ya uzamili ya masuala ya urithi (The International Graduate School: Heritage Studies).
- Ushirikiano katika kuingiza katika ramani maeneo ya urithi wa utamaduni ya mkoa wa Iringa (Joint PGIS mapping) ambapo mradi unashirikiana na kitivo cha Jiografia cha chuo kikuu cha Turku cha nchini Finland pamoja na kitivo cha Jiografia cha chuo kikuu cha Dar esalaam, Tanzania.