Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Iringa Profesa Edward Hosea, alifanya ziara ya kutembelea Makumbusho ya Mkoa wa Iringa Boma, ambayo ni sehemu muhimu ya mradi wa “fahari yetu Tanzania.” Ambao ni mradi uliopo chini ya Chuo Kkuu cha Iringa Katika ziara hiyo, Profesa Hosea alionyesha kujivunia juhudi zinazofanywa na mradi huu katika kukuza vijana katika Nyanja mbalimbali, kuhifadhi utamaduni na kutangaza utalii wa Utamaduni.
Akizungumza katika makumbusho, Profesa Hosea alisema, “Mimi ni mdau mkubwa wa masuala ya utalii. Hongereni kwa kazi yenu ya ukarabati wa jengo hili la kale na uhifadhi uliofanyika mmeweza kurejesha thamani yake, ni wazi kuwa juhudi hizi zina manufaa makubwa kwa jamii na historia ya Tanzania.”
Hata hivyo ameahidi kuunga mkono juhudi zinazofanywa mradi wa “fahari yetu Tanzania” na Makumbusho ya Mkoa wa Iringa Boma, akisisitiza kwamba Chuo Kikuu cha Iringa kitatoa ushirikiano mkubwa ili kuimarisha juhudi za kuhifadhi urithi wa utamaduni.