Mkurugenzi wa fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa – Boma Dk. Jan Kuver akiwa kwenye ziara yake Jijini Dar es salaam alitembelea makumbusho ya Taifa ya Tanzania na kukutana na Mkurugenzi wa makumbusho hiyo Dk. Noel Lwoga.
Kuimalisha mahusiano baina ya makumbusho ya Taifa na Makumbusho zilizo chini ya Taasisi binafsi nimoja kati ya vitu walivyokubaliana wakati wa mazungumzo. Hata hivyo Dk. Noel ameeleza ya kuwa wataitumia siku ya Makumbusho Duniani ambayo huu adhimishwa tarehe 18 mwezi Mei kwa lengo la kukutana na wadau pamoja na Viongozi mbalimbali wa Makumbusho ili kubadilishana uzoefu na kujadili mwelekeo wa sekta ya utalii wa Mambo kale.