Hapo zamani mfumo wa utawala wa kikoloni uliigawa Tanganyika (Tanzania) kwenye majimbo makubwa nane (8), Jimbo la Kusini ambalo lilijumuisha Mikoa ya Ruvuma,Lindi, na Mtwara amabapo makao makuu yalikuwa lindi.
Mwaka 1971 ndipo ulipo anzishwa Mkoa wa Mtwara, kuanzishwa kwa Mkoa huu kulitokakana na mpango wa Madaraka Mikoani ulio simamiwa na Rais wakwanza wa Tanzania Mwl.Julius.K. Nyerere uliokuwa na lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.Tafsiri ya neno “NTWARA” ambalo kwasasa ni Mtwara linatokana na neno la kimakonde “kutwara” lenye maana ya ku-twaaliwa (kuvamiwa na kuchukuliwa mateka).
Asilimia 75 ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara ni Wamakonde. Wayao na Wamakua miongoni mwa makabila yanayo patikana katika mkoa huu. Mradi fahari yetu Tanzania na Makumbusho ya Mkoa Iringa Boma tulifanikiwa kufika Mtwara kwa lengo la utafiti, Mikindani,Mtwara mjini, Tandahimba na Newala ni baadhi ya maeneo tuliofanikiwa kufika wakati wautafiti.