Kutufuatia eneo lilipo, kwa maana ya uwepo wake katika kijiji cha mwisho kabla ya lango kuu la kuingilia mbuga ya Taifa ya wanyama ya Ruaha, pamoja na muundo wa jamii ya makabila mbalimbali yaishio katika eneo hilo kama vile Wamasai, Wahehe na Wabena, kunafanya kijiji cha Tungamalenga kuwa sehemu teule ya mapumziko kwa wanaofanya utalii, kwa kupata burudani na kuangalia shughuli za kitamaduni katika eneo hili. Kituo cha Utamaduni na Utalii cha Tungamalenga sasa kimeendelezwa kwa kushirikiana na Shirika la Uhifadhi Wanyamapori na tayari kuanza rasmi. Pamoja na mambo mengine, kituo pia kimepanga kutoa huduma za kitalii katika maeneo yafuatayo:

  • Huduma za Taarifa kwa Watalii
  • Kutembelea/ Kuoana maisha ya halisi ya wakazi wa eneo hili  (kama vile Boma la wamasai, Ukulima na, maeneo ya kuabudu)
  • Kutembelea katika eneo la usimamizi wa wanyamapori (WMA)
  • vyakula na vinywaji
  • Huduma za choo
  • Kupiga kambi/malazi
  • Muziki wa kitamaduni/maonesho ya ngoma
  • Kuonesha na kuuza bidhaa za utamaduni
  • Eneo la mikutano
  • Fursa ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa vyuo
  • Kituo cha jamii cha utafiti