Mradi wa fahari yetu Tanzania umesaidia na kuchangia matembezi ya kitaaluma ya siku nne ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wanaosoma Shahada ya kwanza ya Utamaduni Antropolojia na Utalii kozi ya uhusiano wakimataifa, walioenda kutembelea baadhi ya balozi za mataifa mbalimbali nchini Tanzania na baadhi ya ofisi zilizopo Dar es laam, kwalengo lakujifunza kwavitendo.
Baadhi ya balozi hizo ni kama Ubalozi wa Ujerumani, Ubalozi wa Ungereza,ubalozi wa Ufaransa, Ubalozi wa Uturuki, ofisi za Umoja wa Ulaya (EU), ofisi za IMF, Pamoja na kutembelea uwanja ndege wakimataifa wa mwalimu Julius Nyerere.